fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Ifahamu Siku ya Pi (π) Duniani

Ifahamu Siku ya Pi (π) Duniani

Spread the love

Tarehe 14 mwezi wa 3 ndiyo siku ulimwengu mzima unasherekea siku ya Pi. Watu wengi leo wanasheherekea π moja ya alama inayotumika zaidi katika hisabati na nina uhakika hata wewe ndugu msomaji umeisha wahi kutana nayo ama umeishawahi itumia.

Pi ama wakati mwingine huwakilishwa kwa alama ya kigiriki π ni  alama inayotumiwa katika hesabu kuwakilisha uwiano wa Mzunguko wa duara kwa kipenyo chake, yaani kila duara lina uwiano ulio sawa kati ya mzunguko wake na kipenyo na uwiano huu ni sawa na 3.14

SOMA PIA  Bloodhound: Gari lenye kasi zaidi duniani

pi-day siku ya pi

kwanini sherehe hii inasherekewa leo!?

Sherehe hii inasherekewa kila tarehe 14 ya mwezi wa tatu kutokana kwamba na alama hii inathamani ya 3.14159265359 na hivyo ukiandika tarehe ya leo katika mfumo wa kimarekani utaona kwamba tarakimu tatu za kwanza yaani mwezi na tarehe vinaleta thamani ambayo ni sawa na π.

Sherehe hizi zilianza lini kufanyika!?

Sherehe za kwana kufanyika zilifanyika mwaka 1988 na zilikuwa zimeandaliwa na mwanafizikia Larry shaw ambaye pamoja na wafanyakazi wenzie wa maabara ya umma huko San Fransisco walisherekea siku hii kwa maandamano katika maeneo ya maabara hiyo.

SOMA PIA  Intel waitetea Huawei: Nje ya Google fahamu makampuni mengine yaliyoathirika

Mwaka 2009 nchi ya Marekani ilipitisha kuwa siku ya tarehe 14 iwe ni siku ya Pi kitaifa, na mwaka 2014 watu wengi walisherekea mwezi mzima wa 3 kama mwezi wa Pi. Mwaka jana sherehe hii iliadhimishwa siku moja tu katika tarehe kama ya leo ila wapo ambao walifanya maadhimisho kamili saa 9:26:53 a.m na pia 9:26:53 p.m maana muda huo ndio unakamilisha tarakimu kumi ambazo zinaunda 3.1492653 ambayo ndiyo thamani ya Pi.

SOMA PIA  Soko la simu janja limesimama - Watu hawanunui simu janja kwa kasi zaidi kama zamani

Siku hii ya Pi isichanganywe na siku ya makadilio  ya Pi ambayo husheherekwa tarehe 22 mwezi wa saba, hiyo ni siku inayosheherekea makadilio ya Pi katika desimali yaani 22/7.

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania