Japokuwa kamera hizi matumizi yake mengi yamejikita zaidi katika mambo ya ulinzi na usalama na mara nyingi sana hutumiwa na polisi. Hata Youtube kuna baadhi za video zinaonesha polisi wakiwakimbiza wahalifu barabarani.
‘DashCam’ ni ile kamera ambayo inakuwa katika dashibodi ya gari na kurekodi matukio yanayotokea mbele ya gari hiyo. Kamera hizi zimekuwa kama sehemu ya kiburudisho kwa baadhi ya watu …..
Huamini? Kuna baadhi ya video zinatumwa katika mtandao wa kijamii wa Vine zikiwa zimerekodiwa na ‘DashCam’. Video hizi mara nyingi zinakuwa ni za kuchekesha na kama si za hivyo basi zinakuwa ni zile ambazo zimerekodi tukio spesheli kwa bahati mbaya (Mambo ambayo huwa hayajirudii kama awali)…mfano utokeaji wa ajali n.k.
Kwa mfano angalia video hii ya Vine, mtumiaji alishuhudia kimondo kinaingia katika uso wa dunia huko nchini Russia
Kumbuka tuna zile nyakati nzuri sana za kupiga picha tukio hata tukiwa tunaendesha ila kabla hatujafikia mfukoni ili kutoa simu zetu tukio linaisha ghafla na tunashindwa piga picha hizo, ukiwa na ‘DashCam’ itakuwa imerekodi kila kitu.
‘DashCam’ ni ndogo, za aina yake na pia sio zile za kushika na mkono katika kurekodi. Kutokana na jambo hili mtumishi wa Google wa zamani na mwanzilishi wa Android, Andy Rubin amerukia katika kipengele cha ‘DashCam’ kwa kuanzisha kampuni yake mpya inayoitwa ‘Playground’.
Rubin aliweka wazi kuwa kampuni yake inashughulika na maswala ya ‘DashCam’ kama mpango wa biashara mpya kabisa
Rubin pia akaongeza kwa kusema kuwa ‘Hardware’ (Kifaa) mtu ataipata bure — Lakini kumbuka hakuna cha bure katika dunia hii — ‘hardware’ sawa itakuwa bure lakini mtumiaji itambidi awasilishe taarifa zote ambazo zimerekodiwa na ‘DashCam’ hiyo.
Bado haipo wazi nini lengo la kampuni hii kwa kuwapa watu kitu cha bire na kuwaomba kitu ambacho mtu asingeweza kabizi kirahisi. Wakati hili bado halijaelewaka vizuri Bw. Rubin akaongezea kuwa kampuni halifanyi kazi hii tuu – kuna na zingine zinafanyika – alivyoendelea kuulizwa maswali akajibu “Siwezi kuliongelea hili kwa sasa”
Ni jambo la wazi kuwa kinachofanywa na kampuni la Playground ni kubwa kwani hata watu wanaondesha kampuni hilo ni wale waliobobea katika uinjinia na ubunifu wa hali ya juu katika kompyuta.
Kama aliweza kugundua Android ambayo leo tunaringia katika simu zetu basi bila shaka hata katika Playground anaweza akavumbua mambo mengi ya maana. Tuambie wewe unaonaje kuhusiana na jambo hili hapo chini sehemu ya comment. Tembelea TeknoKona Kila Siku.
Vyanzo: BetaNews na Vyanzo mbalimbali