Katika moja ya programu tumishi ambazo watu wanatumia kwa wingi duniani kote ni YouTube ambayo utakubaliana na mimi inaweza kusababisha mtu kupata uraibu wa kuitembelea mara nyingi tuu kila siku.
YouTube imekuwa kwenye maboresho mara kadhaa na kama utakumbuka tulishawahi kuandika kuhusu kuondolewa kwa vitufe vya kupenda/kuchukizwa na kile ambacho kimewekwa na mhusika kwenye chaneli yake. Kipengele hicho kimerudishwa tena pamoja na maboresho mengine.
YouTube ya kwenye iOS na Android imeboreshwa kwa kurahisisha watumiaji wake kuweza kufikia vitufe vya kuweza kuamuru picha jongefu icheze/isimame, kupeleka/kurudisha nyuma, n.k. Utakubaliana na mimi kwamba hapo awali iwapo mtu ana anagalia picha mnato kwenye YouTube ambayo imeenea kioo kizima ili kuweza kusimamisha ama kupeleka mbele au kurudisha nyuma basi ililazima mtumiaji kutoka kwenye mtindo wa kuonekana kioo kizima na kuirudisha katika muonekano wa kawaida.
Ingawa hapo awali vitufe hivyo vilikuwepo kwenye YouTube lakini havikufanya kazi pale ambapo mtumiaji alibonyeza ili kuweza kusimamisha au kupeleka mbele/kurudisha nyuma mpaka pale atakapoifunga ili kuweza kuirudisha katika muonekano wa kaida ndio zoezi hilo liliwezekana.
Maboresho hayo ya kwenye Android na iOS yamekwenda sambamba na kubadilisha muonekano wa ile sura ya mbele wakati mtu anaangalia kitu kilichowekwa kwenye chaneli ya mhusika. Vipi wewe unatumia toleo la karibuni kabisa kwenye simu? Unayazungumziaje mabadiko yaliyowekwa huko?
Vyanzo: Engadget, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.