Bwana Ray Tomlinson mgunduzi rasmi wa teknolojia ya barua pepe afariki dunia akiwa na umri wa miaka 74.
Kuna uwezekano umetumia huduma ya barua pepe kwa miaka mingi bila kumfahamu mtu aliyekuja na njia hii ya mawasiliano.
Marehemu Ray Tomlinson ndiyo aliyekuja na njia hiyo ya mawasiliano mwaka 1971 – ikiwa ni mara ya kwanza kuweza kuruhusu mawasiliano ya meseji kati ya mtu na mtu kupitia njia ya kompyuta kati ya watu waliokatika mifumo tofauti ya kompyuta (servers). Na huu ndio ulioleta utumiaji wa alama @.
Alifariki siku ya jumamosi kutokana na kupata mshtuko wa moyo, ila taarifa rasmi ya kifo chake imetolewa leo hii.
Je teknolojia ya barua pepe itakuja kupotea?
Tayari inasemekana Facebook wapo njiani kuzindua rasmi Facebook for Work, toleo spesheli la huduma ya Facebook kwa ajili matumizi ya ofisi n.k
Ingawa ukuaji wa mitandao ya kijamii na huduma za kuchati za kimaofisi kama vile Slack zilionekana kwa wengi zitapunguza au kuathiri teknolojia ya barua pepe ukweli unaonekana si hivyo. Bado barua pepe kwa mabilioni zinatumwa na kupokelewa duniani kote na inaonekana ni teknolojia itakayoendelea kuwa muhimu miaka kwa maka.