fbpx
Nokia, simu, Uchambuzi

Nokia 7.2: Simu mpya ya Nokia inayokuja na kamera ya megapixel 48

nokia-7-2-simu-mpya-kamera-ya-megapixel-48
Sambaza

Simu ya Nokia 7.2 ipo njiani kuingia sokoni na inakuja ikiwa na moja ya kamera ya kiwango cha juu katika simu janja kwa sasa.

Kampuni ya HMD Global inayotengeneza simu za Nokia na kumiliki hatimiliki ya kutumia jina hilo imezidi kujikita katika kuhakikisha wanatengeneza simu zenye kiwango cha hali ya juu. Baada ya mafanikio ya simu yao ya Nokia 7.1 sasa toleo jipya la 7.2 lipo njiani.

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Ku'Block Simu Katika iOs Bila Ya Kutumia App! #iPhone

Mmoja wa wafanyakazi wa juu katika kampuni inayotengeneza vipuri vinavyotumika katika simu ya Nokia 7.2 alitweet kimakosa picha za simu hiyo na hivyo kutoa uhakika juu ya taarifa zinazohusu kamera yake.

nokia 7 2
Tweet rasmi iliyoenda hewani kimakosa

Simu hiyo inakuja na kamera tatu zikiwa na sensor za aina tofauti ili kuhakikisha ubora wa picha zake.

Nokia 7.2
Muonekano wake

 

Taarifa zingine kuhusu simu hiyo zilizovuja mpaka sasa;

  • Inakuja na display/kioo cha HD kwa kiwango cha 1080p
  • Prosesa ya Qualcomm Snapdragon 660
  • Kamera ya Megapixel 48
  • Betri la mAh 3,500
  • Kuna matoleo ya RAM ya GB 4 na GB 6, pia kwenye ujazo wa diski kuna GB 64 na la GB 128
INAYOHUSIANA  Facebook katika ulimwengu wa mahaba

Bado HMD Global hawajatoa taarifa rasmi kuhusu kuanza kupatikana kwa simu hiyo madukani, ila inategemewa ni jambo watakalolifanya mapema mwezi wa tisa na itaanza kupatikana mapema baada ya hapo. Bei pia bado haijawekwa wazi pia.

Tutaweletea taarifa zaidi zitakapowekwa wazi na HMD Global.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |