fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
IPhone simu

Njia Hii Itaongeza Ujazo Wa Uhifadhi (Memory) Katika Simu Yako Ya iPhone!

Njia Hii Itaongeza Ujazo Wa Uhifadhi (Memory) Katika Simu Yako Ya iPhone!

Spread the love

Mara kwa mara nimekuwa nikishauri kama wewe ni mtumiajia wa iPhone basi epuka kununua zile zenye GB 16 kwani hizo GB huwa hazitoshagi sana kwa simu janja kama hizi. Sawa nimekuwa nikisemaga hivyo lakini kuna wengine wanazo na wakifuata njia hii, wataifurahia

Njia hii kwa mara ya kwanza kabisa imegunduliwa na kuwekwa wazi katika mtandao wa Reddit. Wengi walioipokea nia hii kwa tabasamu kubwa ni wale ambao wana simu za GB 16, sawa hata kwa simu zenye ujazo mwingine njia hii inaweza ikafanya kazi

Naongea sana eeh? Haya ngoja tujionee jinsi tunavyoweza kupata ujazo wa uhifadhi wa ziada.

Nenda Katika Settings
Hapa itakubidi uenda katika ‘settings’ ili kujua umebakiwa na kiasi gani cha ujazo wa uhifadhi katika simu yako. Fanya hivi kwa kwenda kwenye Settings > General > About. Shuka chini mpaka kwenye Available ili kuona kiasi cha ujazo kilichosalia.

ujazo

Kiasi Cha Ujazo Kilichobakia

Fanya Kama Unaazima Sinema (Movie)
Usishtuke, utakuwa huazimi sinema kama unavyofikia. Nenda katika sehemu ya iTunes Store na kisha tafuta sinema ambayo ina ujazo mkubwa kuliko ule uliouacha katika simu yako. Ukitaka kufanikiwa jambo hili kwa haraka itakubidi utafute (search) sinema ambazo zina matolea mengi kwa mfano sinema ya Lord Of The Rings.

Fanya Kama Unaazima Sinema

Fanya Kama Unaazima Sinema

Pale utakapojaribu kuichukua siinema hiyo, utapa ujumbe ambao unasema kuwa huna ujazo wa kutosha ili kuichukua sinema hiyo. Ujumbe huo utakuwa umeambatana na machaguo mawili ambayo ni ‘OK’ na ‘Settings’

Ujumbe Utakaopokea Baada Ya Ujazo Wako Ukiwa Hautoshi Kuazima Sinema Husika

Ujumbe Utakaopokea Baada Ya Ujazo Wako Ukiwa Hautoshi Kuazima Sinema Husika

Nenda Tena Katika Settings
Kwa kubofya katika chaguo la ‘settings’ utaenda pale ambapo ulitoka mara ya kwanza. Cha kushangaza ni kwamba utaona muda huu kuna kiasi Fulani cha ujazo kimeongezeka ambacho ni tofauti na mwanzo wakati unaanza zoezi hili

Kiasi Kilichoongezeka

Kiasi Kilichoongezeka

Kinaweza kikawa kimeongezeka kwa kiasi kidogo sana lakini ukifanya njia hii mara kwa mara (mara nyingi) ujazo huo utaongezeka sana mpaka utafikia sehemu utakuwa hauongezeki tena.

SOMA PIA  Vaio Waja Na Simu Janja Yenye Mfumo Wa Android!

Nini Hasa Kipo Nyuma Ya Pazia Kwa Jambo Hili?
Hapa ishu iliyopo ni kwamba ukifanya zoezi hilo simu yako (iPhone) inakuwa inafuta baadhi ya data kama vile zile za ‘Cache’ na zingine nyingi ili kutengeneza uwanja mkubwa wa ujazo wa kukuwezesha kulipia bidhaa husika (Sinema).

SOMA PIA  Google Pixel 5a 5G itatoka mwaka huu

Kwa kutumia njia hii mpaka App zingine zinakuwa zinatumia kiasi kidogo katika kuhifadhi data. Kuna walioshuhudia App ya iTunes Store ikiwa inaandika ‘Cleaning’ (kwamba inajisafisha ili kupunguza data zisizokuwa na muhimu). Cha msingi ni kwamba simu inakuwa inasafisha taarifa ambazo sio za muhimu katika App tofauti tofauti katika simu.

SOMA PIA  Google kuacha kutoa masasisho kwenye simu janja mbili!

Mpaka sasa nna imani utakuwa hutumii njia ya kufuta App zako unazozipenda ili kupata nafasi ya ziada kuweka App zingine unazozipenda zaidi. Kwa kutumia njia hii unaweza ukahifadhi vitu vyako vingi kama vile picha n.k. Kuna waliojaribu njia hii ikawaongezea mpaka GB 3.8 za uhifadhi

Wewe umeipokeaje hii, hebu ijaribu kisha nitonye sehemu ya comment hapo chini. Kwa maujanja kama haya na zaidi ya haya tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku, Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe KatikaTeknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

TeknoKona Teknolojia Tanzania