fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Gari

Donald Trump Ameingilia Mpango Wa Kampuni La Ford Wa Kufungua Kiwanda Mexico!

Donald Trump Ameingilia Mpango Wa Kampuni La Ford Wa Kufungua Kiwanda Mexico!

Spread the love

Kampuni la magari maarufu, Ford limeweka wazi mipango yake ya kufungua kiwanda kikubwa cha kuzalisha magari madogo huko Mexico. Ford tayari imetenga kiasi cha dola bilioni 1.6 za kimarekani kwa ajili ya kuliwezesha hili

Kiwanda hicho kama mikakati yake ikienda vizuri kitaanza kuzalisha magari mwaka 2018. Japokuwa kampuni lina mikakati mizuri lakini bado mkakati wao huo unapata wakati mgumu baada ya kupata changamoto kubwa baada ya watu wengi ikiwemo mgombea urahisi kupitia chama cha ‘ republican’, Donald Trump

Donald Trump anaona mpango huo mzima kama upuuzi tuu na amesema kama akifanikiwa na akashinda kama Rais basi kamwe jambo hilo hataliruhusu.

Kampuni la Ford kwao wanaona ni jambo jema kufungua kiwanda hicho kwani mpaka kufikia mwaka 2020 tayari kampuni litakuwa limeshatengeneza ajira 2,800 – ukiniuliza mimi hii ni namba kubwa sana ya ajira kwa kiwanda kimoja — mpango huu unaaminika kuwa ambao utafanya kampuni liweze kutengeneza magari magodo madog (bei ya chini)

Japokuwa kampuni halijaweka wazi kuwa ni aina gani za magari ambayo yatakuwa yanazalishwa katika kiwanda hicho. Raisi wa ‘United Auto Workers’ (UAW), Bwn Dennis Williams amesema kuwa uwamuzi wa kampuni hilo kufungua kiwanda huko mexico sio mzuri kwani kampuni lingeweza kufungua kiwanda US na wakazi wa marekani wakafaidika na nafasi za ajira kutoka katika kampuni hiyo.

“Makampuni yamekuwa yakikimbilia katika nchi ambazo zina nguvu kazi ya chini na yakimaliza kutengenza bidhaa zao yanarudi nyumbani (US) kuja kutafuta soko. Hili linabidi likome” – aliongezea Bw. Williams

Bw. Trump Akiwa Pembeni Ya Logo Ya Ford

Bw. Trump Akiwa Pembeni Ya Logo Ya Ford

Bw. Trump amekuwa akipinga vikali kwa makampuni ambayo yanataka kuwekeza nchini Mexico akiwa anaamini kuwa nchi yao ya nymbani itakosa mapato makubwa

SOMA PIA  Sweden Imefungua Barabara Ya Umeme (eHighWay) Kwa Magari Makubwa!

Kama akipata uraisi ameahidi atahakikisha hakuna biashara itakayofanyika kwani anaweza akaizuia. Licha ya hayo yote kampuni la Ford bado limesimama katika misingi yake ile ile ya kufungua kiwanda hicho nchini Mexico.

Kampuni imeongezea kuwa sio kwamba nchi hiyo (Mexico) ina nguvu kazi ya hali ya chini bali hata upatikanaji wa malighafi zingine ni rahisi sana na kikubwa ni kwamba wana sapoti kubwa kutoka katika serikali yao.

SOMA PIA  Toyota Wanatengeneza Magari Yanayopaa Kwa Ajili Ya Olimpiki 2020!

Pia kampuni ya Ford imesema isingependa kuonekana kama inaisaliti US kwani kuanzia mwaka 2011 mpaka 2015 ilikuwa tayari imeshawekeza Dola bilioni 10 za kimarekani ambazo zilitengeneza kazi 25,000 kama kazi ambazo ziliongezeka.

Kwa mtazamo wako kama mwana Teknolojia, je wewe unaona nani yuko sawa? Niandikie sehemu ya comment hapo chini. Kumbuka kutembelea mtandao wako wa TeknoKona kila siku kwa habari za kiteknolojia. Pia Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania