fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Nguo Teknolojia

Ujio wa Nguo zinazojisafisha Zenyewe: Hautaitaji Kuzifua tena! #Teknolojia

Ujio wa Nguo zinazojisafisha Zenyewe: Hautaitaji Kuzifua tena! #Teknolojia

Spread the love

Ushawahi kufikiria uwezekano wa uwepo wa nguo zinazojisafisha zenyewe? Yaani suala la kufua linakuwa historia..wanasayansi wamefanikiwa kutengeneza marighafi ya nguo yenye uwezo wa kujisafisha yenyewe na kujitoa uchafu pale inapopata mwanga.

Nguo chafu

Nguo chafu: Huko mbeleni mtu hataitaji kufua tena nguo.

Marighafi (textile) hiyo ya nguo imechanganywa na vidude vidogo (nanostructures) vyenye uwezo wa kuvunja vunja kitu chochote kilicho ‘organic’ (yaani kikaboni/kilichotoka kwenye kitu kilichokuwa hai).

Uvunjaji huo unaotokea pale marighafi hiyo inapokutana na mwanga ndicho kinacholeta usafi kutokea, kwani uchafu uliokuwa umekaa kwenye nguo usika utakuwa umevunjwa vunjwa na hivyo kupotea – kupitia kuanguka – kupeperuka n.k.

nguo zinazojisafisha zenyewe -nanotechnology-self-cleaning-cloths

Kushoto: Muuonekano wa nyuzi za pamba (cotton) zilizofunikwa na ‘nanostructure’ ambazo hazionekani kwa macho ya kawaida – na hapa picha imekuzwa mara 200. Kulia: Muonekano wa ‘nanostructures’ zilizosambamba na pamba – hapa picha imekuzwa mara 150,000 ili kuweza kuonekana

Huu ni utumiaji wa teknolojia ya Nano (Nanotechnology), ambayo kwa kutengeneza vitu viduchu vinavyoweza changanywa na ‘material’ ya nguo. Mwanga wa taa au jua utasababisha nguo ianze kuuharibu uchafu wowote ulio juu yake.

Wanategemea kutengeneza vitambaa kwa ajili ya kushonea nguo vya pamba vitakavyokuwa vimechanganywa vizuri na mjumuiko wa ‘nanostructures’ zenye uwezo wa kujisafisha pale zinapopata mwanga.

Wanasema ni mapema mno kuona nguo za namna hizo zikipatikana madukani ila ni teknolojia wanayoifanyia kazi na tayari ni jambo linalohusu maboresho zaidi. Hasa hasa kuzidi kuhakikisha pia gharama za teknolojia hiyo zinakuwa ni za chini tuu.

Teknolojia hii inatengenezwa na timu ya wanasayansi wa chuo cha nchini Australia – RMIT University.

SOMA PIA  Simu janja Samsung Galaxy M52 5G ipo karibu kutoka

Je unamaoni gani juu ya teknolojia hii ya nguo zinazojisafisha zenyewe?

Soma pia – LAUNDROID: Panasonic Waja na Roboti kwa Ajili ya Kufua, Kukunja na Kupanga Nguo

Chanzo: IBTimes UK  na vyanzo vingine mbalimbali

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania