Wakati dunia ikiwa inajiandaa kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 shirika la habari la Uingeleza lilipata pigo kubwa baada ya tovuti yao kubwa kushambuliwa na wadukuzi (hackers).
Shambulio hilo ambalo lilianza Alhamisi asubuhi liliufanya mtandao huo usiweze kupatikana kwa watumiaji wake.
Inaaminika kwamba shambulizi hilo la mtandao linalojulikana kama DDOS(distributed denial of service) ndiyo lilikua linasabisha mtandao usipatikane kwa kuuongezea mzigo kushinda ambao unaweza kuhimili.
Shambulio hili lilisababisha mtandao huu usiwe hewani kwa muuda wa karibu saa zima uliwafanya watumiaje wake kupeleka lawama zao katika mitandao ya kijamii. Hata hivyo shambulio hilo la kimtandao lilizezwa kuzuiliwa na mtandao ukarudishwa katika hali ya kawaida ingawa hakurudia hali yake ya kawaida kwa asilimia 100.
DDOS ni shambulio la mtandao ambalo haliitaji ujuzi wa udukuzi bali linahitaji kuwa na watu wengi ambao wote wanataka kufungua mtandao mmoja na kuufanya mtandao kushindwa kufunguka. Kwamba kilichofanyika ni kikundi fulani cha watu kilikua kinalazimisha kufungua mtandao huu kwa wingi na hatimaye kuufanya mtandao ushindwe kufanya kazi na kwenda offline.
Kwa kipindi cha masaa kadhaa asubuhi ya Alhamisi mtandao wa BBC News, iPlayer, iPlayer Radio na huduma zingine zinazohusiana nazo zilikuwa hazipatikani. Mtumiaji akitembelea huduma hizo alikuwa anapata ukurasa wa ‘Error 500’.
Hata hivyo mtandao huo kwa sasa umerudi kwa kiasi kikubwa japo kurasa nyingine hazifunguki kwa haraka kama ilivyokuwa kawaida.
Kundi la udukuzi/hack la Anonymous limehusisha na jambo hilo. Hii ni kutokana na kundi hilo hivi karibuni kuitaka BBC wasimfukuze kazi mtangazaji maarufu wa kipindi cha masuala ya magari cha Top Gear, bwana Clarkson.
Jiunge nasi katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, na Instagram
No Comment! Be the first one.