Kabla ya janga la virusi vya Corona lililoikumba dunia nzima matumizi ya programu wezeshi-Zoom yalikuwa yanaonekana kuwa muhimu kwa watu walio maofisini, majumbani lakini jambo la msingi ni kwamba haikuwa na watumiaji wengi kama ilivyo hivi sasa.
Kama ilivyo kwenye nchi nyingi duniani, matumizi ya Zoom yamekuwa makubwa katika kufanikisha wafanyakazi kuendelea kutimiza majukumu yao, wanafunzi wanapata elimu mtandao kupitia kwa walimu wao jambo ambalo limesababisha programu wezeshi husika kuboreshwa mara kwa mara ili kuziba mianya ambayo inaweza kuleta sifa mbaya kwa kampuni inayomiliki Zoom na ni wazi kuwa imekuwa msaada mkubwa ulimwenguni.
Katika maboresho ambayo Zoom imeyafanya ni kuongreza kupengele muhimu kabisa kiitwacho Single Sign-On (SSO) kinachoruhusu wanafunzi kuingia kwenye akaunti zao mara moja na kupata yale yote ambayo yamewekwa huko na walimu wao.
Njia mpya ya walimu/wanafunzi kuweza kuingia kwenye akaunti zao.
>Hili linawezekana kwa mwalimu husika kutengenezea kila mwanafunzi anayepaswa kuhudhuria somo fulani kwenye darasa lake kisha kuwapa walengwa ambapo itawasaidia kuingia mara moja kupata masomo yao lakini pia kutokuwa na hofu ya kukosa vipindi kwa sababu ya kusahau jina maalum na nywila.
>Kwa mwanafunzi ambae ametumia njia ya SSO kuingia kwenye darasa ndani ya Zoom atatambulika kwa jina ambalo mwalimu wake amemsajili,
>Kwa kutumia njia hii inaongeza ulinzi kwa kuwa na wale waliolengwa tu kwani ni wale tu ambao watakuwa na akaunti maalum walizotengenezewa na mwalimu ndio wataweza kuingia kwenye darasa la mtandaoni na
>Njia hii haihitaji mwanafunzi kutumia jina maalum/nenosiri ili kuweza kuingia kwenye akaunti yake ya Zoom.
Kipengele kipya cha kuingia kwenye akaunti ya Zoom kwa njia rahisi.
Ni wazi kwamba usalama mtandaoni unahitaji sana hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari kwa kujihami kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu mtandao iliyo bora.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
No Comment! Be the first one.