Kama inavyojulikana kuwa MS word ni programu muhimu na inayojulikana kuliko zote katika maswala ya kuandika. pengine ni sawa kufikia kiwango hicho kwa kushuhswa. lakini bado changamoto inakujaga kwani App nyingi ambazo sio zile za mitandao ya kijamii huwa zinapata shida sana kufikia kupakuliwa hadi mara bilioni moja
Ms Word bado inajulikana kwa kiasi kikubwa kwani imeweza kujikita kuwa namba moja kwa muda mrefu na kitu kingine ni kwamba Ms Word haijapata mshindani wa dhati ambae anaweza wafanya watuamiji wengi kuhamia kwake.

Ms Word kwa microsoft ni App ya kwanza kuweza kuvuka namba hizo za kushushwa hivyo inakua ni ya kwanza kuweka rekodi hiyo. Lakini ishu nyingine inakuja kuwa kuna baadhi ya simu kama vile baadhi ya Samsung zinakuja zikiwa na hiyo App ya microsoft kuwa katika simu janja hizo.
Hii ina maana gani? hii inaamisha kuwa namba hiyo ya watu walioshushwa ni kwamba kuna baadhi ya namba ya watu tayari walikuta App hiyo katika simu zao mpya tayari.
Kingine kizuri ni kwamba App hiyo katika Playstore inapatikana bure katika soko hilo maarufu la playstore, na kama kawaida cha bure na kizuri huwa kinapendwa sana hivyo basi hata namba ya kushushwa lazima iwe kubwa.

Ukiangalia kwa jicho la tatu hii ni nzuri kwa kampuni kwani ndio App yake ya kwanza kuweza kushushwa katika App store zaidi ya mara bilioni moja na kwa jambo hili wanahitajai peongezi