Kwa miezi kadhaa sasa watumiaji wa intaneti wamekuwa wakiongelea toleo jipya la PS4 ambayo inasemekana itakuwa ndogo zaidi kuliko toleo la hivi sasa iliyopewa jina la “Sony PlayStation 4 Neo”.
Toleo hilo jipya la PS4 litakuwa na muenekano wa picha bora zaidi na pia itakuwa na CPU ambayo itakuwa na kasi zaidi (2.16GHz) kutoka 1.16GHz kwenye toleo la sasa la PS4 pia inasemekana itakuwa na uwezo wa kusupport “Ultra HD Blu-ray playback (4K)”.
Aidha Microsoft nao wanasubiriwa watatoa nini baada ya toleo jipya la PS4 kutoka. “Xbox One” ni toleo lililo chini ya Microsoft ambayo bado haina nguvu ukilinganisha na toleo la hivi sasa la PS4 ambapo Microsoft wanashauriwa kuifanyia maboresho Xbox One.
Yahoo Tech walitoa taarifa hivi karibuni wakisema Sony hadi sasa zaidi ya PlayStation 4 milioni 40 zimeuzika, ukilinganisha na milioni 21 kwa toleo la XBox One.
Kwa habari za hivi karibuni zinasema Microsoft watatoa kifaa cha kucheza game mwakani ambacho kitasupport kifaa cha kuvaa kwenye macho kiitwacho “Oculus Rift” huku Sony wakisema kuwa tutaona ujio watoleo jipya la PS4 baadae mwaka huu ambazo zitakuwa na ukubwa wa kutunza data mpaka 2TB.
Pia, itakuwa ni ndogo, nyembamba zaidi kuliko toleo la sasa hivi na pia kuna uwezekano PS4 Neo itauzwa pamoja na kifaa cha kuvaa kwa ajili ya kuongeza uhalisia cha PVR (Virtual Reality). Kwa muda mrefu Sony wamekuwa wakitengeneza kifaa hicho kwa ajili ya kifaa chake cha magemu cha PlayStation.
Kwa bei na taarifa zaidi endelea kutembelea TeknoKona.com na tutakupa taarifa mara moja pale PlayStation 4 Neo itakapoanza kupatikana rasmi.
Vyanzo: Mitandao