fbpx

Facebook kuja na sarafu yake ya kidijitali mwaka 2020

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mtandao maarufu wa kijamii, Facebook umetangaza kuingiza sokoni sarafu isiyoshikika. Tangazo hilo kutoka Facebook linasema sarafu hiyo mpya ya kidijiti itakayoingizwa sokoni mwaka 2020 inaitwa ‘Libra‘.

Taarifa hiyo imesema baada ya kuingizwa sokoni sarafu yake ya kidijitali ya kidijitali utakwenda sambamba na ujio wa mfuko maalum wa kuhifadhia sarafu hiyo na unaitwa ‘Calibra‘. Hata hivyo, watu wengi wanatia shaka iwapo Facebook wataweza kuitoa sarafu hiyo katika muda alioupanga kutokana na kuanza kuwekewa ugumu na mamlaka mbalimbali nchini Marekani kuhusiana na usalama wa taarifa za watu pamoja na mambo mengine ambayo yanaonekana kuwa bado hayana majibu.

sarafu yake ya kidijitali

Inaelezwa kwa watakaotumia sarafu ya Libra itawawezesha kuokoa pesa lakini  pia mtu kuweza kumtumia mwingine fedha.

Vilevile, wapo ambao wameweka wazi kuisaidia sarafu hiyo ya kidijiti mara tu itakapotoka kutokana na kwamba wanaamini Facebook wataweza kuifikisha Libra sehemu stahiki na kuwa moja ya sarafu zitakazoleta ushindani sokoni. Mbali na hilo zipo taarifa kuwa Facebook kupitia sarafu yake ya kidijitali itaweza kutumika katika mifumo ya malipo kama vile VISA na Mastercard.

INAYOHUSIANA  Facebook Messenger kuwa ndogo zaidi na mambo mapya yapo njiani. #Apps

Facebook imesema kwamba sarafu pamoja na mfuko wake vitaweza kutumiwa na mtu yeyote ambae kwenye simu yake ana programu tumizi za Facebook Messenger, WhatsApp au ‘Calibra. Unaizungumziaje taarifa hii na hasa kutokana na ukuaji wa teknolojia yenyewe?

Vyanzo: CNBC, Gizmodo

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.