Pengine mwaka huu simu janja nyingi za kujikunja zitatoka, Mpaka sasa zimeshatoka nyingi na Motorola Razr toleo lingine la kujikunja linakuja.
Kwa sasa kifaa hiki kinazunguka katika mitandao – kikionekana kwa muonekano wake – na jina lake ni Motorola Razr 40 Ultra Fold.
Uzuri wa kifaa hiki kwa muonekano kinaonekana kuwa na kioo kikubwa ukilinganisha na toleo la zamani.
Rangi ambazo zinakuja katika simu hii ni tatu –bluu, nyekundu na nyeusi— na picha zake zimetoka katika mitandao kadha wa kadha.
Simu hii inakuja ikiwa na kioo cha nje kikiwa ni kikubwa zaidi na hata cha ndani ni kikubwa pia ukilinganisha na toleo la zamani.
Kwan je kwenye kamera kuu ziko mbili huku pembeni yake kukiwa na flash, na kwa ndani kuna kamera moja ya selfi ambayo iko ndani ya kioo.
Prosesa ya simu hii ni ile yenye teknolojia ya Snapdragon 8+ Gen 1 na simu hii inategemewa kabisa kuingia sokoni katika mwezi juni.
Ni wazi kwamba makampuni mengi yanataraji kutoa simu janja za aina hii hivi karibuni, Google wao wameshatoa ya kwao, Samsung wanasubiriwa kwa hamu.
Kwa sasa katika mtandao zimesambaa picha kwa wingi huku wengi wakisubiria siku ya uzinduzi wa simu janja hii ili kujua sifa zake za undani, kaa nasi tutakusogezea hapa hapa.
Je uko tayari kuachana na simu janja zingine na kuanza kutumia simu janja hii kutoka kwao Motorola, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment. Ningependa kusikia kutoka kwako!
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.