Xiaomi 14 Series zinasubiriwa kwa hamu katika soko na kwa taarifa zilizopo ni kwamba simu janja hizi zitaingia rasmi katika soko ifikapo oktoba 27.
Xiaomi ni moja kati ya kampuni ambalo linaleta mapinduzi ya hali ya juu katika swala zima la simu janja maana vifaa vyake vinasifika sana.
Licha ya hayo yote bado kampuni inafanya vizuri katika soko hivyo basi hali hiyo inawafanya kushika namba za juu kabisa katika orodha ya simu janja ambazo zinafanya vizuri.
Fununu tunazisikia tokea muda kwamba kampuni itakuja na matoleo ya muendelezo huo wa 14 na itakua na chipu ya Qualcomm Snapdragon 8 Gen 3.
Simu ambazo zipo katika muendelezo wa Xiaomi 14 na zinategemewa kutoka ni nne ambazo ni Xiaomi 14, Xiaomi 14 Pro, na Xiaomi 14 Ultra.
Kama ilivyo iPhone 15 Pro Max hata Xiaomi 14 Pro inategemewa kuwa na jumba la Titanium na uwezo wa kuungaishwa na satellite
Kamera ya simu hizo itakua ni ile ya Leica ambayo kwa sasa inasifika sana na makampuni mengi yanaitumia na yanapata sifa nyingi sana katika nyanja hiyo.
Ni wazi kabisa kwamba simu hizi zitakua na ushindani mkubwa sana kwa simu ambazo zitakua katiak soko kwa kipindi cha muda huo ambapo zitatoka
Kuhusiana na sifa za undani hilo bado halijawekwa wazi pengine siku ya utambulisho ndio mambo yatawekwa hadharani kwa kila mtu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ushawahi kutumia matoleo ya simu za kampuni hii., je matoleo haya yakoje? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.