fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Samsung wazindua Galaxy M42 5G

Samsung wazindua Galaxy M42 5G

Wiki hii imekuwa na mambo mbalimbali yayohusu Samsung ambao wamezindua bidhaa zao kadha wa kadha tayari kwa ajili ya sisi watumiaji duniani kote. Rununu ama simu janja Samsung Galaxy M42 5G tayari imeshazinduliwa!.

Samsung ambao wamekuwa wakiendelea kutoa bidhaa mbalimbali za kidijiti wameona inafaa kuleta Galaxy M42 5G ambayo kimsingi inavutia kutokana na kuja na kile ambacho soko inahitaji kwa sasa. Pata kuzifahamu sifa za rununu husika.

Memori :
 • Diski uhifadhi: 128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka TB 1
 • RAM: 6GB/GB 8
Kamera :
 • Kamera Kuu: MP 48, 8, 5 na 5+taa mbili za kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu
 • Kamera ya Mbele: MP 20
Kipuri mama :
 • Snapdragon 750G

Programu Endeshi

 • One UI 3.1, Android 11
Rangi/Bei :
 • Nyeusi na Kahawia
 • GB 6/128-$295 (zaidi ya Tsh. 678,500) na GB 8/128-$322 (zaidi ya Tsh. 740,600) bei ya ughaibuni

  Galaxy M42 5G

  Rununu hii pia imewezeshwa Samsung Pay, teknolojia ya Knox mahususi kwenye ulinzi wa kifaa husika. Ina uwezo wa kudumu na chaji kwa saa 130 ikihusisha kusikiliza muziki tu.

Simu hii itaingia sokoni Mei Mosi kwenye masoko mbalimbali ya mtandao kama Amazon, Samsung wenyewe. Sasa ni wewe msomaji wetu kufanya maamuzi yako kujipanga kuinunua au la!

Vyanzo: Gadgets 30, GSMArena

SOMA PIA  Asus Zenfone 6: Simu ya kamera mbili kwa moja
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania