Baada ya miaka 10 ya kuiongoza Vodafone hatimae mkurugenzi mkuu Vittorio Colao ametangaza rasmi kuwa kuachia ngazi kuiongoza kampuni hiyo.
Vittorio Colao amekuwa mtu muhimu sana ndani ya Vodafone kwa miaka ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kuuza sehemu ya hisa zake kwa kampuni ya Verizon Wireless ya Marekani kwa thamani ya Dola 130 bilioni. Colao ataendelea kusalia katika nafasi yake mpaka mwezi Oktoba wakati Nick Reed (mkurugenzi wa masuala ya fedha) atakapochukua nafasi yake.
Mchango wa Vittorio Colao kwa Vodafone.
Vodafone ni moja ya kampuni kubwa za mawasiliano kutoka nchi ya Uingereza inayofanya vizuri sehemu mbalimbali duniani.
Bw. Colao alijiunga na kampuni ya Vodafone mwaka 2001 na alipitia katika ngazi tofauti tofauti za uongozi akifanya kazi katik nchi kama vile Misri, Australia na Qatar. Mkuu huyo aliyeng’atuka hivi karibuni (kabla ya kuachia ngazi) amefanikisha Vodafone kuinunua Liberty global kwa $21.8bn jambo ambalo lilikuwa likitegemewa kwa muda mrefu tu.
Katika robo ya nne ya mwaka ulioisha mapato ya Vodafone yamepanda kwa 11.8% na kufikia Euro 14.7bn; wataalamu wa masuala ya fedha walitabiri kampuni hiyo ingepata kiasi cha $14.6bn sawa na 10% lakini kampuni ikipata ongezeko la asilimia 1.1 kulinganisha na ilivyokuwa imetabiriwa.