Siku hizi, kutumia skrini zenye vitufe ni jambo la kawaida kiasi kwamba ni vigumu mtu kurudisha mawazo kwa siku ambazo njia pekee ya kutumia kompyuta ilikuwa skrini nyeusi au bila skrini kabisa. Wakati Windows 3.0 ilipotoka kwenye mwaka 1990, lilikuwa toleo la windows lililoshika kwa kasi zaidi ya ilivyowahi kutokea, watu wengi hawakujua jinsi ya kutumia kipanya (‘mouse’) wala skrini ya kisasa (‘GUI operating system interface’).

Ili kuwazoesha watu na kuwafundisha kutumia kipanya, Microsoft waliamua, baadala ya kutumia miongozo, watumie magemu (michezo) kujifunzia kutumia vipanya. Windows 3.0 ilikuja na gemu za Solitaire na Reversi. Magemu haya yalisaidia sana watu kujizoesha kutumia vipanya na hasa Solitaire ambayo ilimtaka mchezaji akamate kadi na ‘kuiburuza’ na kudondosha inapotakiwa kuenda (‘drag and drop’)- jambo ambalo lilikuwa muhimu kwenye utumiaji wa Windows.
Ufundishaji wa GUI kwa staili hii haukuishia na Windows 3.0, kwani kwenye toleo lililofuata la Windows 3.1, mchezo mwingine ukajitokeza: Minesweeper. Kama Solitaire ilivyowafunza watu kutumia kipanya ‘kuburuza na kudondosha’, Minesweeper ilitilia mkazo kwenye kutumia kitufe cha kushoto, kulia na cha kati kwenye kipanya, jambo ambalo liliwafanya watu waizoee zaidi kipanya cha kisasa.
Chanzo:HowToGeek
No Comment! Be the first one.