Ni wazi kwamba kuna simu janja za aina nyingi sana na pengine nchini china ndipo kunapoongoza kuzalisha simu nyingi tena za aina tofauti tofauti mfano mzuri ni simu za Meizu.
Meizu ni simu ambazo zinatengenezwa huko china japokua soko lake kubwa ni nchini humo lakini bado unaweza ona matoleo yake katika mataifa mengine.
Kwa taarifa ambazo tumezipata ni kwamba kampuni hiyo itazindua matoleo ya simu hizo ndani ya mwezi huu wa tatu.
Utambulisho wa vifaa hivi kwa dunia utaambatana na uzinduzi mkubwa kabisa ambao utafanyika katika ukumbi wa Shanghai Mercedes-Benz mnamo tarehe 30 mwezi machi mwaka huu.
Ukaichana na matoleo ya Meizu 20 ambayo yatatambulishwa siku hiyo, bado kutakua na utambulisho wa vitu vingine
Katika matoleo ya simu janja hizi ni kwamba Kuna teknolojia, Flyme 10, na Flyme Auto ambazo zinatumika katika magari na zinatokanaa kabisa na simu hizi
Ukiachana na hayo ni kwamba kampuni ya Lynk & Co nayo itatambulisha biadhaa zake ambazo zitatambulishwa katika jukwaa hilo hilo.
Kwa sasa watu wanaweza weka order zao ili simu zikitoka tuu wazipata na kwa kaisi kikubwa kwa nchini china jambo hili linaweza kufanyika kwa watu kutemebelea maduka yanyojulikana kama Meizy Mall.
Matoleo mapya yatajumuisha matoelo mbalimbali ya Meizu 20 na Meizu 20 Pro. Ukiachana na kwamba sifa za undania kabisa za simu hizi hazijawekwa wazi, lakini inasemekeana kwamba zitakua na sifa ambazo zitakua zina ushindani mkubwa kwa simu ambazo zipo sokoni.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unahisi simu hii kama aikitoka je itakua ni tishio kubwa kwa simu ambazo zina majina makubwa na zinalitikisha soko? Niandikie hapo chini katika eneo la uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.