fbpx
Android, simu, Tecno, Uchambuzi

Ifahamu Simu ya Tecno R6 LTE! #Uchambuzi

ifahamu-simu-ya-tecno-r6-lte-uchambuzi
Sambaza

Moja ya makampuni ya simu nchini Tanzania ambayo yamekuwa mstari wa mbele kuuza simu kwa bei ya promosheni basi huwezi kuacha kutaja kampuni ya Tigo. Leo ifahamu simu ya Tecno R6 LTE ambayo inapatikana kwenye maduka yake.

Simu janja zimekuwa na umaarufu mkubwa na kutokea kuteka soko la simu sehemu nyingi duniani, katika miaka ya karibuni ni nadra sana kumuona mtu akiwa na simu ya kawaida na pembeni asiwe na simu janja. Moja ya simu janja ambazo zipo katika soko la simu janja kupitia makampuni ya simu nchini Tanzania ni Tecno R6 LTE.

Je, Tecno R6 LTE ina sifa zipi?

Simu janja zinazouzwa kwenye maduka ya mitandao ya simu mara nyingi zinakuwa na zenye uwezo wa kawaida ili kuweza kuhakikisha zina bei ambayo ni rafiki kwa wateja wengi zaidi. Zinakuwa na uwezo wa kufanya kazi zote kwa yule mtumiaji asiyependa ‘makuu’ kwenye simu janja.

 1. Prosesa/RAM. Moja ya kiungo muhimu sana kwenye simu ni uwezo wa prosesa na RAM kwa sababu vipengele hivi viwili ndio vitatoa picha kamili iwapo simu husika itakuwa na kasi wakati wa ufanyaji wake wa kazi. Tecno R6 LTE ina prosesa ambayo kasi yake ni 1.3GHz. Uwezo wa RAM katika Tecno R6 LTE ni GB 1 tu.
 2. Ukubwa wa kioo/Programu endeshaji. Kama wewe si mpenzi wa simu janja ambazo zina vioo vipana basi Tecno R6 LTE itakufaa kwani kioo chake kina ukuwa wa inchi 5.5 na ubora wa chochote kinachoonekana kwenye uso wa kioo hicho ukiwa ni 540×960pixels. Inatumia programu endeshaji yenye watumiaji wengi sana duniani, hapa nikimaanisha Android 7.0 Nougat.

  Tecno R6 LTE: Muonekano wake kwa mbele na nyuma.
 3. Kamera/Diski uhifadhi. Kipengele kingine kinachowavutia wateja wengi wa simu janja ni kwenye upande wa kamera na diski uhifadhi; Tecno R6 LTE ina kamera mbili na ile ya nyuma ina MP 8 kuongeza MP 2 za kwenye flash mbili kwa nyuma na kamera ya mbele ina MP 5. Dski uhifadhi wa ndani ni GB 16 lakini ikiwa na uwezo wa kukubali ujazo wa ziada wa mpaka GB 32.
 4. Betri/Rangi. Tecno R6 LTE ina betri ambalo haliwezi kutoka huku likiwa na uwezo wa 3,000 mAh aina ya Lithium-Polymer. Simu hii inapatikana katika rangi mbalimbali kama vile dhahabu, fedha na kahawia.

Sifa nyinginezo za Tecno R6 LTE

Kwa upande wa ulinzi inatumia alama za vidole, inatumia laini 2 (kubwa na ndogo), uzito wake ni gramu 190, mfuniko wake wa nyuma ni wa plastiki, kioo chake ni ule muundo ambao umejikunja kidogo (curved).

Undani wa Tecno R6 LTE: Simu hii ni ya mwaka 2017.

Katika vipengele  vilivyopewa alama za juu kabisa (8/10) ni upande wa usikivu wa simu na upande wa intaneti; ukitaka kuchapisha kitu kwenye mtandao ina kasi ya 5.76 Mbps huku ukitaka kupakua kitu kutoka mtandaoni ina kasi ya 21 Mbps.

Tecno R6 LTE ni inatumia mfumo wa 3G tu na bei yake si kubwa, ni Tsh. 195,000 katika maduka ya Tigo.

Je, huwa unanunua simu kwenye maduka ya simu Tanzania? Ni simu gani umeshawahi kununua au unapanga kununua? Tuandikie hapo chini kwenye sehemu ya maoni.

Chanzo: PDevice

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Instagram Waleta 'Instagram Direct'; Onesha Picha Kwa Chaguo Lako
1 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

 1. Ifahamu Simu ya Tecno R6 LTE! #Uchambuzi – TeknoKona Teknolojia Tanzania
  January 30, 2018 at 10:35 am

  […] post Ifahamu Simu ya Tecno R6 LTE! #Uchambuzi appeared first on TeknoKona Teknolojia […]