LG walitangaza simu ya hali ya juu iitwayo G4 mwezi wa 4 na sasa wametangaza G4 Beat, simu ya hali ya kawaida inayotokana na G4.
G4 Beat itatumia Android Lollipop 5.1.1 na itakuwa na prosesa ya Snapdragon 615 pamoja na GB 1.5 za kumbukumbu na GB 8 za uhifadhi wa ndani. Itakuwa na kioo chenye ukubwa wa inchi 5.2 HD, ambayo ni ndogo kidogo ya G4 yenyewe ila ina ujazo wa pixeli wa ppi 423.
Sifa nyingine:
- Kamera kuu: MP 8 (na MP 13 kwa nchi nyingine)
- Kamera ya mbele: MP 5
- Rangi: Fedha, Nyeupe na dhahabu
Pamoja na kuwa na kamera yenye sifa nzuri, kamera ya G4 Beat inatangazwa kuchukua baadhi ya teknolojia kutoka kwenye G4 kubwa kama uwezo wa kuchukua rangi ya picha inayofaa zaidi kwa kutumia sensa ya rangi (‘colour spectrum sensor’), inatangazwa kumpa chaguzi nyingi mtaalamu wa masuala ya upigaji picha kuamua picha itokaje na pia itaweza kurahisisha upigaji selfie kwa kutumia ishara.
G4 Beat itaanza kupatikana baadaye, mwezi huu na LG watatangaza bei yake katika kila soko muda huo.
Kusoma uchambuzi wa simu mbalimbali tembelea pia ->
Chanzo: theNextWeb
No Comment! Be the first one.