fbpx
simu, Tanzania, Teknolojia, Uchambuzi

Walemavu wa kusikia na matumizi ya simu Tanzania

walemavu-wa-kusikia-na-matumizi-ya-simu-tanzania

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Lugha za alama/mtindo wa kutumia maandishi ndio njia rahisi ya kufanya mawasiliano na mtu mwenye ulemavu wa kusikia popote pale duniani lakini inawezakuwa changamoto tena sio ndogo iwapo nyenzo hizo hazipo hivyo kusababisha mgongano wa lugha.

Ulemavu wa aina yoyote ile sio kitu kizuri na upo katika makundi mbalimbali. Binafsi suala zima linalogusa mlemavu daima huwa linanikereketa na kila kiungo ni muhimu katika mwili wa binadamu LAKINI kwa maoni yangu yeyote mwenye ulemavu wa macho kwangu mimi naona amepoteza kiungo muhimu sana hasa upande wa milango mitano ya fahamu ingawa makala hii inalenga kundi jingine la watu wenye ulemavu.

Ukiniuliza ni kundi gani la watu wenye ulemavu Tanzania limeachwa nyuma basi sitasita kutaja watu wenye ulemavu wa kusikia na hii inatokana na mifano dhahiri ambayo haina ubishi mathalani uwasilishwaji wa habari kwa kundi hilo la watu wenye mahitaji maalum, mahospitalini, ofisini, shuleni, n.k na si kwa sababu wataalamu hakuna, la hasha! Bali watu wenye ulemavu wa aina hiyo ni kama wamesahaulika.

INAYOHUSIANA  Teleprompta: Teknolojia ya kusoma habari katika televisheni na hotuba za viongozi

Dunia ya leo imetawaliwa na teknolojia nawengi wetu tunafahamu mbinu ambazo unaweza ukazitumia kuwasiliana na walemavu wa kusikia kwa ujumla wao na pengine wengi wetu tunahofia kuwapigia simu kwa hofu kuwa hamtaelewana, hapana mimi nakataa. Hii inatokana na kuwepo na simu ambayo inaweza ikabadilisha kile unachokisema na kukiweka katika lugha ya maandishi na mhusika akaweza kuelewa kikamilifu sababu ya wewe kumpgia simu. Teknolojia hii imekuwepo tangu miaka ya 1960 na tangu hapo imekuwa ikiboreshwa.

Walemavu wa kusikia
Simu ya kisasa mahususi inayoweza kurahisisha mawasiliano baina ya watu lakini mmojwapo akiwa ni mlemavu wa kusikia.

Kwanini nimechagua simu ya mezani?

Kutokana na ukuaji wa teknolojia simu za mezani zimesahaulika kwa wengi wetu lakini ni kitu ambacho kinaweza kuwa msaada sana majumbani, kazini ausehemu yoyote ile ambapo watu wa aina mbalimbali wanaingia na kutoka. Ofisi, mashirika, benki, hospitali, sehemu zenye mkusanyiko mkubwa wa watu nlemavu wa kusikia anapata shida sana kuweza kupata huduma kutokana na yule anayezungumza nae hawaelewani sababu kuu ni KUTOKUJUA LUGHA ZA ALAMA/UTOKUWEPO KWA NYENZO RAFIKI ZINAZOWEZA KUTUMIWA NA MLEMAVU WA KUSIKIA.

Je, wajua?!

Neno “deaf” na “Deaf” kwa maana ya kwamba ni mlemavu wa kusikia ni maneno mawili yanayozungumzia ulemavu wa aina moja lakini wa viwango tofauti. Fahamu ya kuwa iwapo utakutana na sehemu pameandikwa “deaf” maana ya ni mtu huyo amepoteza uwezo wa kusikia ukubwani kutokana na umri mkubwa, hajui lugha za alama, anapenda kupata uwezo wa kusikia tena kama ikiwezekana.

Deaf” ni neno linalomaanisha mlemavu wa kusikia LAKINI ambae ni mwanachama wa chama cha watu wenye ulemavu wa aina hiyo (CHAVITA-Kwa Tanzania),  anajua lugha za alama na hata pengine ni mfanyakazi, anaweza kutumia teknolojia saidizi zinazomuwezesha kuwa na uwezo wa kusikia na amepata ulemavu wake ni wa asili (alizaliwa nao).

Walemavu wa kusikia
Ukitaka kuwa karibu na mtu mwenye ulemavu wa kusika basi wewe pata kujua lugha za alama.

Makampuni, taasisi, mashirika, CHAVITA lugha za alama ni lugha kama nyingine yoyote ambayo mtu anaweza kujifunza na isitoshe ni taaluma, watu wanajifunza, kufaulu na kuhitimu sasa inakuaje mnashindwa kuwa na wataalamu wa aina hiyo ili kuhudumia kundi fulani la walemavu ambalo haliangaliwi kwa jicho la karibu?

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Wizara husika na serikali kwa ujumla kama mna uwezo wa kutoa amri na ikafuatwa inakuaje inashindikana kulazimisha kampuni zinazotoa huduma ya habari kuwa na wataalamu wa lugha za alama ili basi kundi hilo lenye mahitaji maalum uweza kujua kinachoendelea?. Tubadilike, wataalamu wapo wengi tu kama zilivyo kada nyingine.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|