fbpx

Leseni za WhatsApp Kenya: Wamiliki makundi ya WhatsApp watakiwa kuwa na Leseni

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Katika kudhibiti majukwaa ya mitandao ya kijamii, watawala nchini kenya wamependekeza muswada ambao utawalazimisha watu walioanzisha makundi ya WhatsApp, Facebook na Wanablogi kuwa na leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano ya Kenya.

Muswada huo ambao tayari umeshapelekwa Bungeni unataka Viongozi (Administrators) wa makundi ya WhatsApp kuwa na leseni na kuwasajili wanachama (Members) wa kundi na pia kujua anuani zao za mahala wanapoishi.

INAYOHUSIANA  Tuzo ya mwaka kwa Tecno Phantom 8

facebook whatsapp apps leseni za whatsapp

Na pia kuweka wazi kile kinachojadiliwa ndani ya kundi kwa jeshi la polisi. Kiongozi wa kundi atalazimika kujaza majina ya wanachama wake pamoja na anuani zao wakati wa kujaza fomu maalumu ya kupata leseni ya uendeshaji wa kundi lake.

Pia Viongozi hao watatakiwa wawe na wanachama waliofikia miaka 18 au zaidi.

Endapo muswada huo utapita basi yeyote atakayeendesha Kundi bila ya Leseni atakumbana na adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja Gerezani au faini ya Kshs 200,000/- (Takribani Tshs 400,000/- )

Soma habari mbalimbali na maujanja ya app ya WhatsApp hapa -> Teknokona/WhatsApp

Aidha wanablogi watakaoendesha Blogu zao bila ya Leseni watapigwa faini ya Kshs 500,000 (Takribani 1,000,000/-) au kifungo cha miaka miwili gerezani.

Muswada huo unatarajiwa kusomwa Bungeni wiki ijayo.

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.