fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

apps Microsoft Windows

Toleo la Kivinjari cha Microsoft Edge chenye misingi ya Chromium lavuja

Toleo la Kivinjari cha Microsoft Edge chenye misingi ya Chromium lavuja

tecno

Tayari habari ya ujio wa kivinjari cha Microsoft Edge kinachotengenezwa kwa kodi ya msingi ya Chromium ilitangazwa na Microsoft. Toleo la beta la kivinjari hichi limevuja na sasa linapatikana mtandaoni.

Chromium na Chrome kivinjari

Kushoto: Logo ya Chromium, Kulia: Logo ya Google Chrome.

Chromium ni mradi wa utengenezaji wa kivinjari huru kinachokuja na teknolojia za kisasa zaidi za mtandao. Mradi huu unasimamiwa na Google na unahusisha wadau wengine wowote wanaojisikia kuchangia. Kupitia toleo la Chromium ndio Google anaboresha na kuingizia manjonjo kadhaa kuleta toleo la Google Chrome. Kwa wengi uamuzi wa Microsoft unaonesha Google imeshinda kiteknolojia katika eneo la teknolojia za vivinjari.

kivinjari cha Edge kinachotumia kodi mama ya kivinjari cha Chromium

Muonekano wa kivinjari cha Edge kinachotumia kodi mama ya kivinjari cha Chromium

 

SOMA PIA  FAHAMU: Huduma Ya 'Live Location' Ni Nini Katika WhatsApp Na Jinsi Ya Kuitumia!

Microsoft hatakuwa wa kwanza kuachana na utengenezaji binafsi wa kivinjari na kutegemea kivinjari kikuu cha Chromium katika kuleta toleo lake la Kivinjari cha Edge, tayari miaka mingi sasa ata kivinjari cha Opera kinatengenezwa juu ya misingi ya Chromium.

Sifa na uwezo wa toleo la Edge havijaenda mbali na sifa zilizokuwa zinategemewa kuwepo kwa kivinjari kinachotengenezwa juu ya kivinjari mama cha Chromium. Kivinjari cha Edge sasa kitaweza kukubali ongezeka la uwezo (extensions) kwa kupakua plugins kutoka moja kwa moja kwenye soko la Chrome la Google – ingawa pia kutakuwa na soko la extensions la Microsoft.

Muonekano wa Kivinjari cha Edge (Chanzo: The Verge)

Kikubwa wamechukua Chromium na kuipa muonekano mzima wa programu za Windows na kuweka huduma zake za Microsoft kuwa ndio huduma kuu – hii ni pamoja na huduma za kuhifadhi kumbukumbu n.k.

Kwa sasa toleo hili si salama sana kwa utumiaji – kwani lipo kwenye kiwango cha beta. Toleo rasmi likianza kupatikana tunakupa taarifa.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania