fbpx
Apple, apps

Vipya kutoka Apple Machi 2019: Fahamu yaliyojiri

vipya-kutoka-apple-machi-2019

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Vipya kutoka Apple Machi 2019: Apple watambulisha mambo kadhaa mapya leo, Jumatatu 25 Machi. Katika shughuli iliyofanyika katika ukumbi wa Steve Jobs ulio kwenye makao makuu ya kampuni hiyo huko nchini Marekani Apple wametambulisha mambo kadhaa. 

Ili kufanikiwa kushindana na huduma kama vile Netflix, Apple wanakuja na show mbalimbali zinazosimamiwa na masupastaa

Hii ni pamoja na huduma ya habari ya kulipia, huduma ya muvi na tamthilia ya kulipia kupitia app ya Apple TV na huduma ya kibenki kupitia kadi ya manunuzi ya Apple Card. Kupitia huduma ya app ya Apple TV Apple wanataka kuwa watengenezaji wa tamthilia, muvi na show mbalimbali – na ili kufanikisha hili wameandikisha tayari watu maarufu/masupastaa kadhaa wa nchini Marekani kama vile Oprah and muigizaji Jason Momoa.

> Apple News+

Vipya kutoka Apple Machi 2019
Apple News+

Kwa dola 9.9 (Zaidi ya Tsh 22,000) kupitia app ya Apple News+ watu wataweza kusoma habari kutoka vyanzo mbalimbali vya habari vya kulipitia kama vile National Geographic, Popular Science, New Yorker, Vogue, Rolling Stone, Times na vingine vingi.

INAYOHUSIANA  Microsoft Apps : Soko la Apps za Microsoft kwa Ajili ya Simu na Tableti za Android

> Apple Arcade

Ulimwengu wa magemu. Apple wametengeneza ulimwengu wa magemu unaokwenda kwa jina la Apple Arcade. Kupitia ulimwengu huu watengenezaji wamgemu wataweza kutengeneza magemu kwa kutumia ulimwengu ambao tayari umetengenezwa na utaendelea kuboreshwa.

Vipya kutoka Apple Machi 2019
Apple Arcade: Kwenye app ya AppStore kutakuwa na eneo jipya kwa ajili ya Apple Arcade

Kutokana na ulimwengu huu magemu yanaweza kutofautiana kutokana na wahusika na maeneo gemu husika limejikita zaidi. Pia gemu litakuwa tofauti tofauti ata kwa watu wawili wanaolicheza.

> Apple TV

Apple wanaleta app ya Apple TV. Kupitia app hii utaweza kupata muvi, tamthilia na chaneli zingine mbalimbali za TV kwa wakati mmoja kupitia app ya Apple TV. Pia utaweza kupata huduma za muvi au chaneli kutoka Hulu,  DirecTV, Prime TV.

INAYOHUSIANA  Facebook : Ndugu na Marafiki sasa kupost kwenye akaunti za Marehemu Facebook
Apple TV

Pia kuna huduma ya kulipia chaneli zile tuu unazozitaka,

Kwa tamthilia unaweza kudownload show unazozihitaji tuu na kuzihifadhi kwenye app ya Apple TV ili uzitazame pale unapotaka. Tofauti na huduma zao zingine ambazo zimekuwa zikipatikana kwenye mataifa machache tuu, huduma ya app ya Apple TV itakuwa inapatikana katika mataifa zaidi ya 100 duniani kote. Kwa kiasi kikubwa wamejiweka katika kutaka kushindana na Netflix.

> Kadi ya malipo – Apple Card.

Apple Card: Ni kati ya malipo ya baada (Credit card).

Katika kitu kipya kinachoonekana kina uwezo wa kufanikiwa sana katika walivyotambulisha basi ni Apple Card. Kupitia app ya Apple Pay, utaweza kuwa na kadi ya malipo ya kidigitali ya Apple Card. Kwa kadi hii utaweza kufanya malipo huduma mbalimbali za kimtandao bila uhitaji wa wewe kutumia kadi yako ya kawaida ya benki. Pia kwa wenye uhitaji wa kadi ya kushikika (physical card) basi app watatoa pia kadi kwa kushirikiana na MasterCard. Kadi ya app tofauti na zingine haitakuwa na maelezo yeyote ya kinamba kwenye muonekano, na itachukua rangi ya dhahabu.

INAYOHUSIANA  YouTube GO - App ya YouTube isiyokula data sana

Tofauti na kadi za kibenki za kawaida kadi ya Apple itakuwa na usiri wa matumizi ya mteja, Apple hawatakuwa na taarifa kuhusu umetumia kadi hiyo kufanya malipo gani – taarifa hii itabaki kwenye app ya Apple Pay unayotumia tuu. Usalama wa kadi hiyo utakuwa umeunganishwa na usalama wa simu yako kupitia usalama wa teknolojia kama Face ID na Touch ID.

Je katika haya kutoka Apple ni kipi unadhani kimekuvutia zaidi?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |