Kivinjari cha Google Chrome chafikisha wastani wa watumiaji bilioni 1 kila mwezi, hawa ni watumiaji wa simu na tableti tu. Google wametoa data hizo katika maadhimisho ya toleo la 50 la kivinjari hicho maarufu.
Ingawa data zilizotolewa na Google hazijaonesha watumiaji wa kivinjari hicho kwenye kompyuta bado inaonekana watakuwa ni wengi tuu, ila siku hizi watumiaji wa mobile (simu na tableti) ndiyo muhimu kwani ndio vifaa vinavyotumika zaidi ya kompyuta.
Data kali zaidi ni hizi;
- Kila mwezi kuna wastani wa kurasa bilioni 771 za tovuti mbalimbali hufunguliwa kupitia kivinjari hicho.
- Pia kivinjari cha Chrome kimesaidia kutunza usalama zaidi ya mara milioni 145 kwa kuzuia tovuti zisizosalama kupakua (download) programu zisizosalama kwenye kompyuta za watumiaji wake.
- Zaidi ya password (nywila) bilioni 9.1 zimehifadhiwa katika mfumo wake wa kusaidia watu kukumbuka password zao.
- Pia Google washalipa zaidi ya dola milioni 2.5 za kimarekani kwa watafiti mbalimbali waliosaidia kugundua na kutoa taarifa zilizosaidia kuboresha usalama wa kivinjari cha Google Chrome
Chanzo: Google blog