Hapo awali Vine ulikua ni mtandao maarufu sana wa kutengeneza video ndogo ndogo zenye urefu wa sekunde 6.
Hii ilikua ni maarufu sana kwani kwa sekunde chache wengi walejitahidi kutengeneza video fupi sana ambazo zilikua zinaleta maana. Nyingi zilizopendwa zilikuwa ni zile za kuchekesha.
Twitter ilinunua mtandao huo wa Vine na lengo lake kubwa kupitia mtandao huo ilikua ni kuona kuwa jamii ya wana Twitter wanautumia mtandao huo kwa ajili ya kudumisha ubunifu wa kujitegemea kwa watumiaji. Lakini kwa sasa mambo si mambo, mambo yanenda vibaya katika kampuni ya Twitter.
Kwa mtazamo wa kampuni ya Twitter ni wazi kwamba imeona kuwa mtandao huo kwa sasa hauna faida kwa kampuni kwani mpaka sasa twitter imeweka wazi plani zake za kuuzima mtandao huo katika miezi ijayo.
Kingine cha kushangaza ni kwamba kampuni ya Twitter imesema kuwa licha ya kuupiga chini mtandao huo lakini bado itahakikisha kuwa inaacha App na ‘Website’ ya vine kuendelea kutumika. Yaani mtu utaweza kuangalia Vine zote mpaka kufikia kufungwa kwa mtandao huo (kwa lugha nyingine ni kwamba utakuwa na uwezo wa kuangalia vine za zamani tuu).
Taarifa zilizopo ni kwamba kampuni halijatoa sababu juu ya kwanini wamefikia maamuzi hayo. Kumbuka vine ikifa inamaanisha wafanya kazi wengi sana watakosa kazi? Swali ni je wataajiriwa Twitter? Subiri kabla hujajibu hilo kumbuka pia katika Twitter na kwenyewe mamia ya kazi yanapunguzwa? Umekosa jibu sasa sio?
Twitter iliichukua Vine mwaka 2012 na kuiachia rasmi januari 2013 na hapo ndipo mtandao ulipojipatia umaarufu mkubwa. Kibaya ni kwamba kadri siku zilivyozidi kwenda na umaarufu ukawa unashuka. Kibaya zaidi ni pale mtandao wa Instagram ulipokuja na huduma ya video mwaka 2013 ndio kabisa watu wakaanza kusahau Vine.
Twitter hawajatoa siku maalumu ya kuupumzisha kwa amani (kuachana nao) mtandao huo wamesema tuu “miezi ijayo” hivyo basi kaa karibu na TeknoKona kwani tutakujuza kila linaloendelea.