fbpx

Jinsi Ya Kulazimisha Kushusha Gemu Ya ‘Pokemon Go’ Kwa Android Na iOS!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Pokemon Go ni mchezo wa simu (Android na iOS) ambao umejipatia umaarufu kwa kipindi cha muda mchache sana. Pia ndio mchezo unaoongoza kushushwa kwa haraka kwa kipindi cha muda mfupi

Ukiachana na hili pia inaweza ikawa ndio mchezo wa kwanza kutengeneza pesa nyingi kwa muda mchache. Mpaka sasa mchezo huo piku na kuweka historia kadhaa.

pokemon go

Pokemon Go

Japokuwa umekua ni maarufu sana lakini bado haupatikani katika sehemu nyingi duniani. Mfano Tanzania bado mchezo huu haujaanza kupatikana katika masoko ya simu janja. Je unataka uupate?

Fuata Nyayo Hizi

Kwa Watumiaji Wa Android.

Kama umezunguka katika soko la Google PlayStore na ukaukosa basi hauna jinsi inabidi uushushe kupitia njia nyingine mbadala (Japokuwa njia hii si salama kwa asilimia 100)
Kwanza hakikisha sehemu ya ‘Unkown Sources’ katika settings za simu yako ya android imechaguliwa.

Sehemu Ya 'Unkown Sources' Katika Settings Za  Android

Sehemu Ya ‘Unkown Sources’ Katika Settings Za Android

Baada ya hapo ingia katika Pokemon Go APK Webpage ili kushusha faili ya APK la mchezo huo na kisha lishushe. Likikamilika kushuka ingia ili kulipakua katika simu yako na baada ya hapo unaweza ukalifungua ili kuanza kucheza.

INAYOHUSIANA  Alama 'Kidole Chini' a.k.a 'Dislike' Haitakuja Facebook ~ Zuckerberg

Kwa Watumiaji Wa iOS.

Njia hii ni tofauti kabisa na hiyo ya Android hapo juu, kama una uhakika gemu hii (Pokemon Go) haipo katika nchi yako unaweza ukafuata njia hizi ili kuipata.

Pokemon Go

Pokemon Go

Cha kwanza kabisa inakubidi uwashawishi Apple kwamba upo katika eneo ambalo wanaruhusu gemu hiyo kupatikana.

Ili kufanya hivyo inakubidi kuingia katika sehemu ya settings katika kifaa chako cha iOS na kisha ‘Log/Sign Out’ katika akaunti yako ya Apple ID.

INAYOHUSIANA  Spika za masikoni kuchuja hewa chafu

Kisha rudi katika eneo la Settings na kisha chagua General > Language & Region. Chagua eneo lako kama US, New Zealand au hata Australia.

Baada ya hapo fungua App Store na kisha tafuta Pokémon Go na itatokea. Kama haitatokea hapo kama App ya bure kushusha usiwe na hofu chagua ‘Create New Apple ID’

Fanya zoezi zima la kufungua akaunti mpya ya Apple ID na katika sehemu ya njia ya malipo chagua ‘None’ na kisha weka Us, New Zealand au Australia kama eneo lako unaloishi.

INAYOHUSIANA  TCRA: Tarehe ya kuzimwa simu feki haitasogezwa mbele

Ukishamaliza zoezi hilo basi hapo unaweza ukashusha gemu la Pokemon Go kiulaini kabisa (haaha) na kuanza kulicheza.

Pokemon Go

Pokemon Go

Pokemon Go

Pokemon Go

Mchezo Mwema!

Nigependa kusikia kutoka kwako, wapi umekwama, Je umeweza kulishusha? Niandikie sehemu ya comment hapo chini. Tembelea TeknoKona kila siku kwa maujanja na habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.