Mtandao wa kijamii wa Instagram ambao una umaarufu mkubwa sana Afrika mashariki upo njiani kubadilisha namna tunavyoona posts walizoweka rafiki zetu katika mtandao huo.
Instagram wanataka kutumia algorithm ambayo itaamua post gani tuzione kwa urahisi zaidi.
Hatua hii inapingwa na watumiaji wengi wa mtandao huo, na kuonesha hasira yao juu ya jambo hili watumiaji hao wameanzisha hashtag ya #ripinstagram ambayo imeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Instagram sio mtandao wa kwanza kuanza kuleta mfumo wa algorithm katika kuonesha post katika timeline, Facebook walianza mnamo mwaka 2009 ambapo walibadili mfumo ambao ulikuwa unamuwezesha mtumiaji kuona post katika mtiririko ule ule ambao zilipostiwa na badala yake wakaleta algorithm ambayo huchagua zile post ambazo inadhani wewe unapenda kuziona kutokana na aina ya marafiki ulionaonao.
Twitter nao pia walitangaza kuanza kutumia mfumo huu mapema mwezi wa pili mwaka huu walitangaza kufuata nyayo za Facebook na kuleta mfumo wa algorithm, Twitter pia kama ilivyokuwa kwa Facebook watumiaji walipatwa na hasira na wengine walitishia kuuhama mtandao huu iwapo kama wangeaza kutumia huduma hiyo.
Instagram nao wameamua kuleta mabadiliko hayo inayoonekana kwa kiasi kikubwa ni kwa ajili ya kuongeza mapato ya matangazo zaidi. Kwani hadi sasa ilikuwa ni rahisi sana makampuni kufikia watumiaji wanaowafollow bila ata ya kutumia pesa – ukilinganisha na Facebook ambapo ata kama page inamashabiki (fans) 100,000 post ya kampuni itawafikia watu wachache sana kama pesa ya kujitangaza haitatumika.
Nini hasa kinabadilika katika Instagram?
Ipo mifumo miwili ambayo inatumika kukuonesha kile ambacho marafiki zako wamekipost ukurasa wa Kijamii.
Mfumo wa kwanza ni ule ambao unahakikisha kwamba unaona post zote kama ziliivyowekwa yaani kama mimi nilipost picha saa5 kamili asubuhi halafu rafiki zako wengine x na y wakapost picha tuseme x alipost saa6 na y alipost saa7 basi wewe utakapofungua mtandao huo saa 7 utaona picha kutoka kwa y aliyepost saa 7 kisha utaona ya x aliyoipost saa 6 na mwisho kabisa utaona post ya kwangu, njia hii huitwa reverse chronological order na ndio njia inayotumiwa na Instagram kwa sasa.
Mfumo wa pili na ndio ambao Instagram wanataka kuhamia huu unatumia algorithim kuamua post ipi uione ya kwanza katika timeline yakwako, tuchukue mfano kwamba una marafiki wanne w,x,y and z, tuseme w ametuma picha saa 5 ,x saa6 ,y saa 7 na z saa 8 kwa mfumo mpya ambao instagram wanataka kuhamia basi algorithm itaangalia katika hao marafiki wako yupi awe wa kwanza katika orodha bila kujali kwamba yupi alikuwa wa kwanza kupost picha.
Wanaoipinga haya mabadiliko haya wanasema kwamba hatua hiyo ya Instagram itakuwa ni kuingilia uhuru wa watumiaji kwa kuwapangia mambo ya kuyaona.