Google Glass, teknolojia na bidhaa ambayo wengi walioona imewahi kuletwa na Google kabla ya muda wake na hivyo kutokuwa na maana sana kwa sasa imeboreshwa na bado Google waanaamini kuna sehemu inaweza tumika – makazini.
Google Glass ni kifaa kama miwani kinachompatia mvaaji wake uwezo wa kusoma taarifa mbalimbali kupitia kioo chake na pia ata uwezo wa kurekodi mambo huku kikiwa na mawasiliano ya moja kwa moja na simu janja ya mtumiaji wake.
Wazo la kwanza kwa Google la bidhaa hii ni kutumika na watu wa kawaida katika mizunguko yao ya kila siku. Fikiria badala ya kusoma sms au ujumbe wako mpya kwenye app iliyo kwenye simu yako – kupitia Google Glass uweze kusoma moja kwa moja bila kutoa simu yako mfukoni.
Kutokana na sababu mbalimbali bidhaa hii ilionekana kama vile imekuja wakati usio wake na wengi kuona kifaa hichi kinaingilia ‘privacy’ za watu wengine – hii ni kutokana na uwezo wa wewe kurekodi mambo bila ya wengine kujua.
Google wakakaa kimya kwa muda mrefu na wengi wakajua bidhaa hiyo ndio imepotezewa ila kumbe Google walikuwa wanakuna kichwa jinsi ya kuiboresha na kutafutia matumizi yanayoweza kubalika zaidi. Vitu vilivyoboreshwa kwa sasa ni pamoja na uwezo wa kukunja na kukunjua kama vile miwani za kawaida, na pia maboresho yamefanyika kuongeza muda wa kukaa na chaji.
Google wameona kwa sasa kuna namna nyingi zaidi Google Glass inaweza tumika maeneo ya kazi. Kwani kupitia Google Glass inakuwa rahisi mtu kupata data flani kwa uharaka zaidi bila ya uhitaji wa mfanyakazi husika kufungua kompyuta yake au kupitia makaratasi. Kwa sasa Google wanatengeneza Google Glass kwa kufikiria huitaji wa wafanyakazi wa kampuni au mashirika husika wanaohitaji.
Inategemewa kifaa hichi kitaweza kuwa muhimu katika maeneo kama mahospitalini, mashuleni na viwandani.
Kwa sasa jina la utani la programu hii ya utengenezaji wa Google Glass mpya unafahamika kama Google Glass EE yaani Google Glass Enterprise Edition kuweka msisitizo ya kwamba sio tena bidhaa ya mtumiaji wa aina yeyote.
No Comment! Be the first one.