fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Facebook

Facebook Waja Na Safety Check!

Facebook  Waja Na Safety Check!

Spread the love

safetycheckmobielcarousel

Kampuni nguli inayohusiana na mitandao ya kijamii Kupitia mtandao wao wa Facebook, imekuja na ‘tool’ mpya inayoitwa ‘Safety Check’ambayo inaweza kutaarifu familia na marafiki kwamba mtumiaji yupo salama. Facebook itatumia maeneo (location) katika maprofile ya watu ili kuangalia nani atakua hatarini. Pia itatumia watu waliokaribu (Nearby Friends) na watu wa eneo hilo kwa ujumla wanaotumia Mtandao kwa mda huo.

“Katika kipindi cha migogoro Mtandao unaweza kuwa ndio njia kubwa ya kuwasiliana na watu wa karibu na kusambaza taarifa kwa ujumla” alisema CEO Wa Facebook Mark Zuckerberg

hero_phone_1x-screen1-engMaafa yakitokea ‘Safety Check‘ inatuma meseji kwa wale wenye App  ya facebook kwenye simu zao kuwauliza kama wako salama (Are You OK?)  Mtumiaji anaweza amua chagua nipo salama (Im Safe) au Sipo katika eneo hilo (Im Not In The Area) na Itawajulisha marafiki na familia.

Wazo la Safety check lilizanza baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 2011 na Tsunami iliotokea Japan. Mainjinia wa Facebook waliunda bodi ambayo ilisaidia kusambaza taarifa za majanga hayo na watu kuwasiliana. Hawakuishia hapo bodi iliendelea fanya kazi mpaka kufikia Safety check.

SOMA PIA  Uwezo wa DAIMA kunyamazisha vitu kwenye WhatsApp

Blog ya Facebook ilisema “Katika majanga hayo tuliona watu walitumia mitandao ya kijamii na teknolojia kwa ujumla ili kuwasiliana na wale wanaowapenda na kuwajali”

laptop_iphone_lower_2x_cv1

Safety check ipo tayari kama kuna maafa yoyote  na itapatikana dunia nzima kwenye Store Za iOs na Android kupitia Aplikeshini ya Facebook  na Hata kwenye Kompyuta

SOMA PIA  Facebook: Kuwa na mafariki wengi zaidi ya kikomo

 

Ni vizuri kujua hata mitanadao ya kijamii inajali usalama wa nje wa watumiaji wake. Wewe unaonaje hii, Wazo lao ni zuri sio? maana sidhani kama kuna mtandao mwingine wa kijamii ulio na tool kama hii. Toa mawazo yako kwenye kiboksi cha Comment tafadhali.  

Siku Njema!!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. […] bado huelewi jinsi ya kutumia safety check makala hii hapa itakusaidia jinsi ya kutumia, share na marafiki zako nao waelewe juu ya jinsi ya kutumia huduma hii […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania