fbpx

apps, Facebook, instagram

Facebook kuondoa katazo la matangazo yenye maneno mengi

facebook-matangazo-yenye-maneno-mengi

Sambaza

Kwa muda mrefu tovuti ya kijamii ya Facebook imekuwa ikizuia matangazo yanayolenga kutumika Facebook au Instagram kama yatakuwa na maneno mengi kwenye picha.

Kama sehemu ya utaratibu ya matangazo kwenye mitandao hiyo ya kijamii Facebook walikuwa wanalazimisha wanaotengeneza matangazo ya picha basi kuhakikisha si zaidi ya asilimia 20 ya eneo la tangazo/picha linakuwa na maneno. Ilikuwa kama asilimia ikizidi basi tangazo halitafikia watumiaji wengi au linaweza zuiliwa kabisa kuweza kufanya kazi kwenye tovuti hizo.

Mambo yamebadilika

facebook na instagram matangazo
Facebook na Instagram ni moja ya majukwaa makubwa ya kimatangazo katika sekta ya mitandao ya kijamii. Makampuni na biashara mbalimbali zinategemea mitandao hii kufikia wateja wao

Kuanzia sasa Facebook wamekubali kuondoa katazo la matangazo yenye maneno mengi kwenye picha zinazotumika. Kwa sasa matangazo yenye maneno mengi ndani yake, ata kama ni zaidi ya asilimia 20 ya picha nzima yatafanya kazi kama kawaida – linapokuja suala la uwezo wa kuwafikia watumiaji wa mitandao hiyo maarufu ya kijamii.

Facebook wamesema bado wanaendelea kushauri maneno yasizidi asilimia 20 kwa kuwa mara nyingi matangazo yanayozidi asilimia hiyo utafiti wao unaonesha ndiyo yanayofanya vizuri zaidi. Ila kwa sasa Facebook wameamua suala hili kuwa kama ushauri tuu na si kigezo cha wao kuyazuia matangazo hayo au kuingilia utendaji wake kazi.

INAYOHUSIANA  Line yajitosa kwenye sarafu zisizoshikika

Kwa wanaojishughulisha na uwekaji wa matangazo mtandaoni mabadiliko haya yatakuwa ni habari njema kwao. Kwa sasa watu wataweza kutengeneza matangazo kwa ajili ya mtandao huu maarufu wakiwa huru bila wasiwasi pale ambapo tangazo linahusisha kuwa na mananeo.

Wewe kama mtumiaji wa mitandao ya kijamii, je ni matangazo ya namna gani huwa unayapendelea zaidi? Ya picha au video?

Vyanzo: Facebook & Socialmediatoday
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*