Facebook ni moja kati ya mtandao wenye watumiaji wengi sana. hivi imeshawahi kukutokea ukiwa katika mtandao huo ukashangaa tangazo limetokea na linaendana kabisa na kile ulichokuwa unakiangalia awali au umetoka ku’click’?.
Hapo inakubidi ushtuke kwani ukifuatilia vizuri unaweza kabisa ukasema Facebook inakujua vizuri tuu. Kabla hujakataa ndio! Inaweza ikawa inakujua kwani inafuatilia vitu vingi juu yako kama vile nini unapenda, unaangalia au hata ku’click’ na ni kwamba taarifa kama hizi zinatolewa hata kwa watangazaji
Mtangazaji akijua kitu unachopenda (ambacho Facebook imemwambia) itakuwa ni rahisi kwa yeye kutangaza biashara yako kupitia wewe.
Ukifutalia vizuri sio Facebook tuu ambayo ina taarifa zako na kukufuatilia. Kuna makampuni mengi tuu yana taarifa zako na yamepata kutoka Facebook kwa mfano ni mara ngapi umeingia katika mitandao mbalimbali na ukajiunga katika mitandao hiyo kwa kutumia taarifa zako za facebook (“Sign Up With Facebook”)?
NJIA ZINAZO ONYESHA MAKAMPUNI YANAFUATILIA TAARIFA ZAKO
App Za Facebook: kwa mfano hii inaweza ikakutokea pale rafiki yako katika mtandao huo anakutumia mwaliko wa kujiunga na mchezo (gemu) Fulani na wewe unaamua kujiunga. Kama umeshawahi kufanya hivi basi umewaruhusu wale wenye mchezo huo kuweza kukufuatilia nyendo zako. Japokuwa facebook huwa inakuambia uchague ni kitu gani watu hawa waeze kuona kupitia akaunti yako, lakini nina uhakika ni watu wacheche sana huwa wanafanya hivyo.
Kuingia Katika Mtandao Kupita Facebook: Kama ulishwahi kuingia katika mtandao mwingine na ukakuambia “Log in with Facebook” na kisha wewe ukafanya hivyo basi umeliwezesha kampuni hilo kupata taarifa zako
App Za Marafiki Kukuona: Hata kama hujashusha App hiyo, Kwa kutumia marafiki zako wenye App hiyo, Facebook inaiwezesha App hiyo kukuona kupitia marafiki zako.
Njia Za Kutokomeza Hili
Pitia Na Hariri Tena App Ulizonazo: Ili kuangalia App ambazo umeziweka katika akaunti yako ya Facebook bonyeza katika Menu na kisha nenda katika eneo la ‘Settings’ na kisha chagua Apps
Ili kujua ni taarifa gani App husika inazijua (umeipa idhini ya kujua) bonyeza kialama cha penseli. Ukiwa hapo unaweza ukabadilisha vitu vingi kwa mfano App kama ya Skype inachukua taarifa nzima ya ‘Profile’ lako pamoja na listi ya marafiki zako, namba za simu na hata wanapoishi.
Kumbuka taarifa kama hizi zinakuwa zinahifadhiwa katika ‘Server’ za makampuni mengine kabisa na pia kumbuka sio kila kampuni litakuwa na ulinzi wa hali ya juu kama vile Microsoft. Pia kumbuka wadukuzi wana uwezo mkubwa wa kutumia taarifa ndogo na kufanya kitu kikubwa sana.
Futa App Ambazo Huzitumii: Kama kuna App uliiweka katika Facebook kitambo hicho na sasa huna mpango nayo tena ifute tuu. Hapo utakuwa umeitoa katika kukufuatilia tena. Kwa kufanya hivi haimaanishi kuwa umejitoa kabisa katika App hiyo kwani bado itakuwa na taarifa zako lakini haitaweza kupata taarifa zako zingine (mpya)
Zima Kuwa App kabisa: kwa mfano baada ya kusoma hapo juu ukaamua kufuta App zako zote na katika akili yako ukasema hutakuja kuwa na App tena baasi huna budi kujitoa katika mchakato wa kuweza kupata App nyingine. Kufuta unaweza ukaenda katika Settings>> “Apps, Websites and Plugins,” click “Edit” >>>”Disable Platform”
Ukifanya hivyo pia hii haitafanya taarifa zako kutoonekana kwa wale ambao tiari wanazo. Kitakachofanyika ni kwamba utakuwa huwezi kuingia katika mtandao mwingine kwa kutumia taarifa zako za Facebook na kingine ni kwamba utakuwa huwezi kuingiza App nyingine katika mtandao wako wa Facebook labda mpaka uamue kuwasha tena kipengele hiki.
Acha Ku Log In Kupitia Facebook: Kama umeingia katika mtandao mwingine na umekuambia kuwa unaweza ukajiunga katika mtandao huo kwa kutumia akaunti yako ya facebook kataa, kama utaweza kuendelea tengeneza akaunti katika mtandao huo upya kabida.
Mambo ya kufanya ili kuepukana na majanga haya ni mengi sana lakini yaliyosemwa hapo ni machche ambayo wengi yanawakuta. Ili kupata vitu salama kabisa wakati ukiwa katika mtandao wa Facebook basi Tu Like TeknoKona. SIKU NJEMA!