Baada ya mshikemshike na vikwazo kwa mpango wao wa FreeBasics huko nchini India, Mark Zuckerberg hajakata tamaa. Kupitia mpango wao wa internet.org, Mark Zuckerberg anaendelea na na matumaini yake ya kuunganisha maeneo yasiyofikiwa na intaneti duniani kwenye intaneti, kwa kutumia droni.
Zuckerberg aliandika kwenye ukurasa wake hivi karibuni akisema, “Ninafurahia maendeleo na Aquila, project yetu ya sola inayolenga kutoa huduma ya intaneti katika sehemu zinazopata shida ya intaneti kufika.
“Tumechukua hatua nzuri za uhandisi na kwa miezi mingi sasa, tumeweza kuirusha kila wiki ndege yetu ya majaribio” Aliandika Zuckerberg kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Hii habari ni nzuri kwa nchi zinazoendelea kwani ni maendeleo yanayoweza kuleta huduma ya intaneti kwenye maeneo magumu kufikia. Hata hivyo, mipango kama hii huwa na dhana mbadala ya kufaidisha kampuni husika na kama tulivoona huko nchini India, amabako wanaharakati wengi waliipinga FreeBasics ya internet.org, huenda Facebook wakapata vikwazo tena kwani droni hapa barani Afrika siyo kitu cha kawaida na sheria zake bado ni changa.
Zuckerberg ameweka picha pia za kuonesha jinsi mpango huo unavyoendelea
//
As part of our Internet.org effort to connect the world, we’ve designed unmanned aircraft that can beam internet access..
Posted by Mark Zuckerberg on Thursday, March 26, 2015
Chanzo: TechRepublic, TheGuardian