fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti

Drake Sasa ana ‘Google’ Inayomhusu Yeye Tu!

Drake Sasa ana ‘Google’ Inayomhusu Yeye Tu!

Spread the love

Je, umewahi kuwa na maswali ya kujiuliza kuhusu Drake na ulikuwa unatamaani sana huduma ya kukujibia maswali hayo bila ya usumbufu wa kutafuta muda mrefu? Ombi lako sasa huweza likawa limekubaliwa. Msanii Drake sasa ana ‘Google’ inayomhusu yeye tu!
Huduma hii ya kusaidia kutafuta ya mambo ya Drake inaitwa Let Me Drake That For You au LMDTFY kwa kufupisha- kama Drake mwenyewe anavyopenda kufanya.
Drake amefanikiwa kujipatia umaaufu kwa kuweza kutoa kazi bora kwa muda mrefu bila kuchoka na pengine inawezekana akaingia kwenye historia ya wasanii bora wa muziki huo. Huduma hii mpya ya kutafuta mambo yanayomhusu Drake inamfanya kuwa tofauti kwani ni wazo jipya kwa mtu au kampuni yoyote.
LMDTFY inafanana sana na Google ila tofauti yake ni kwamba LMDTFY inakupa matokeo ya Tweet, habari na post nyinginezo zinazomhusu msanii Drake. Kama kibwagizo, unapomaliza kutafuta kitu flani na kurudi kurasa ya mwanzo wa tovuti hiyo, utasikia ‘Hold on We’re Home’, nyimbo maarufu ya Drake.

Ukurasa wa LetMeDrakeThatForYou ukitafuta 'Drake Hand'

Ukurasa wa LetMeDrakeThatForYou ukitafuta ‘Drake Hand’

Maelezo kwenye kurasa yake inasema kwamba:
“#lmdraketfy ni kama google, bomba zaidi. Tafuta chochote na gundua jinsi kinavyohusiana na Drake. Kila kitu ulichokuwa hukijui na unakihitaji maishani.
Tumekuwa hapa kwa muda mfupi ila tunaendelea kuboresha matokeo ya kutafuta na kuyafanya ya maana zaidi.”drake_hand_22_0_1428588431
Mchambuzi mmoja wa gazeti la Forbes anadhani kwamba tovuti kama hii, ingawa ni kwa kujifurahisha, inaweza kutumika na makampuni kukusanya na kuonesha mambo yanayoihusu kampuni hiyo.

Picha: Getty Images, at40.com

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania