Apple imetangaza rekodi yake mpya kufikiwa, na hii ni juu ya watumiaji wa vifaa hivyo vya Apple kudownload Apps mbali mbali kwa idadi ya takribani bilioni mia moja. Bilioni miamoja ni namba kubwa sana hasa kwa kitu ambacho kilianzishwa mwaka 2008. Ndiio App store ilianzishwa mwaka 2008.
Sio tuu kwamba kuna App bilioni mia zilizoshushwa App store lakini pia Apple imewalipa ‘devolopers’ (waboreshaji) dola bilioni 30 za kimarekani (Kumbuka dola 1 ni takbribani tsh 2000/=). Watengenezaji apps hao wamelipwa kutokana na App store, yaani ni wale wanao miliki App ambazo zinauzwa katika soko la App Store. Soko hili limekuwa ni muhimu na ni sehemu ya kipato kwa developers hao. Apple wamesema mtu wa kawaida anakadiriwa kuwa na App 119.
“App store inampa kila mtu mwanya wa kuweza kufanya vitu mbali mbali na pia kuna kizazi cha aina yake katika watengeneza filamu na watoaji stori kinachokuja” — Alisema muingozaji wa Filamu, J.J. Abrams katika video iliyoandaliwa na Apple katika WWDC
Ndio Sio kwamba Apple ndio kampuni pekee linalomilika Soko la kimtandao juu ya Apps, Hapana bali kuna makampuni mengine makubwa kama lile la Google, Google Play Store. Masoko haya yote yanatoa huduma ya Apps kwa simu zake tuu — mtu wa anaetumia Apple haweza shusha App kutoka Google Play store — Licha ya kuwa Google play ndio inayoongozwa kuwa na App nyingi na ndio inayoongoza kwa App zinazoshushwa lakini bado Apple wanatengeneza hela nyingi kupitia App Store
Kampuni la Apple halionyeshi dalili zozote za kupunguza mwendo kwa sasa kwani hata mauzo ya simu yake mpya ya iPhone yameshangaza kwani ndio mauzo mazuri na ya muda mfupi kuliko matoleo mengine ya iPhone yaliyowahi toka. Yaani iPhone 6 imeingiza matunda (pesa) mengi katika kampuni kwa kipindi cha muda mchache.
Apple pia waliweka wazi baadhi ya vipengele vipya katika iOs na hata katika OS X katika mkutano wa WWDC 2015 huko San Francisco. Tuambie unaonaje mwenendo wa Apple, je wataumaliza mwaka vizuri kama walivyo uanza?
WWDC = World Wide Developers Conference
No Comment! Be the first one.