Kampuni ya Apple inc ya nchini Marekani inayojihusisha na utengenezaji wa bidhaa mbali mbali za Teknologia ikiwa ni pamoja na simu zilizojipatia umaarufu mkubwa zilizopewa jina la iphone imekua na utamaduni wa wakuwaacha midomo wazi watumiaji wa bidhaa zao pamoja na wapinzani kila wanapotambulisha bidhaa au huduma mpya.
Tarehe 4 mwezi huu Apple waliitambulisha na kuinadi Simu ya iphone 4s, simu hiyo haitofautiani muundo na ile iliyoitangulia yaani iphone 4 isipokuwa features zake zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana kuanzia kwenye uwezo wa camera, kasi ya utendaji na hata mfumo “Operating System”.
Moja ya vitu ambavyo vimeteka hisia za wadau wa maswala ya Teknologia pamoja na wapenzi wa simu za iphone kwenye toleo hili jipya (iphone 4s) ni feature iliyopewa jina la “Siri”, hii ni software ambayo inamuezeja mtumiaji wa iphone kuipa maagizo simu yake kwa kutumia sauti (voice commands) kitu hiki si kigeni sana lakini uwezo wa kutambua maagizo na kuyafanyia kazi haujawahi kuwa wa kiwango cha juu kwa kiasi ambacho software ya Siri kwenye iphone 4s imefikia.
Unaweza kutumia Siri kuiagiza simu yako kwa kutumia sauti kufanya chochote ambacho iphone 4s ina uwezo wa kufanya kuanzia kwenye kupiga simu, kutuma ujumbe, kutuma barua pepe n.k, mbali na kutenda kile ulichoiagiza simu yako kufanya “Siri” inaiwezesha simu yako kukujibu kwa sauti na kukueleza kile kinachofanyika. Natumaini umeipata vyema “Siri”.
Endelea kutembelea blog hii ili upate kufahamu features nyingine nyingi za iphone 4s pamoja na mambo mengine mengi.
Mimi sio mdau sana wa apple na products zao, ila nimetokea kuwakubali sana katika hardware design zao, kudos for that. ila apple wanakuwa overrated and hyped kupita kawaida, kiukweli SIRI is the most advanced speech control i have ever seen and that is the best thing for them, ila no one expected after 14months watakuja na gadget almost similar iphone4 with improved perfomance which is no match to most latest android devices. iOS 5 sio the best OS kama wanavyodai na vitu vingi tu ambavyo wamekuwa wakidai kwa muda mrefu, they need to invest kwenye research zaidi to conquer it all
Nimekukubali hapo master, nadhani Android ipo juu zaidi kwa sasa.. Ila apple products huwa zinapata promo zaidi. Nadhani kutokana na Google kununua kampuni ya Motorola tunaweza ona ushindani zaidi siku hizi.
Deal ya motorola na google ipo pagumu sana, kuna issue za anti-trust but i hope itafanikiwa… what i am worried ni kuwa google itakuwa kama apple with their streamline products, ambayo hiyo pia might be bad news to samsung na HTC who sell a lot of android devices… kiukweli without iOS inawezekana tusingeiona Android, or if ingekuwepo ingekuwa totally different, weaknesses za iOS na android ni sawa sehemu nyingi, no deep researches have been done by both, nokia walikuja na what geeks consider the best mobile OS with true multitasking never seen before Maemo 5 and Meego ambazo zote zimekuwa discontinued because of one crazy CEO who worked at microsoft and probably doesn’t wanna see these Linux Mobile OS hitting it hard in the market…. sasa tusubiri tu WP7 vs Android vs iOS….
Yeah, kitu kinachivutia ni kwamba Android in 2 years time imeweza kuwa namba moja katika soko, kwa zaidi ya asilimia 35% ikiachia zingine kwa iphone, blackberry na zingine..