Soko la simu linazidi kukuwa kwa kiasi kikubwa sana, hii inapelekea pia ushindani kuongezeka. Kwa karne ya sasa mpaka simu janja ilishike soko inabidi iwe na mambo mengi ya kipekee.
Ukiachana na simu makampuni mawili makuu ya simu (Apple na Samsung) ambayo ni tishio kwa makampuni mengine bado kuna makampuni yanafanya juu chini ili kuhakikisha yanatawala dunia katika teknolojia ya simu.
Kwa sasa inaonekana dhahiri kuwa watu wanasubiria kwa hamu kuona simu hizi.
1. Google Pixel XL
Simu hii inamilikiwa na kampuni ya Google. Simu janja hii inatoka ikiwa ni toleo baada ya simu za Google zinazojulikana kama Nexus. Simu janja hii inasemekana itakuja ikiwa na programu endeshaji ya Android 7.0 Nougat. Kuijua zaidi simu hii soma hapa.
2. Microsoft Surface Phone
Kumbuka kampuni la Microsoft lilitoa tableti ambazo zinafahamika kama Microsoft Surface (Pro), na sasa imeona haitoshi na kuja na simu za aina ya Surface. Pengine labda hili limefanyika baada ya kuona kuwa zile za Lumia hazifanyi vizuri katika soko.
Kampuni la Microsoft halijatia neno lolote juu ya simu hizi lakini maneno yaliyopo mtaani ni kwamba itakuja ikiwa na jumba la chuma na ‘finger print’ yake itakua kwenye kioo kabisa. Simu hizi zinasemekana kuwa zitatoka zikiwa za aina tatu.
Aina ya kwanza itakuja na RAM GB 4 na GB 64 kama ujazo wa uhifadhi. Ya pili itakuja ana RAM GB 6 na ujazo wa uhifadhi GB 128 na ya tatu itakuja na RAM GB 8 na ujazo wa uhifadhi ukiwa ni GB 512.
Kingine cha kuvutia ni kwamba kamera yake ya mbele itakua na MP 8 na ile ya nyuma itakua na MP 21. Uwezo wake wa betri inasemekana utakuwa ni 3,000 mAh na programu endeshaji itakuwa ni Windows 10 Mobile.
Simu hii inategemea kutangazwa mwanzoni mwa mwaka 2017 au mwishoni mwa mwaka 2016. Kaa karibu na TeknoKona ili kupata taarifa za undani kabisa endapo simu hii itatoka.
3. OnePlus 4
Kampuni ya OnePlus ni moja kati ya kampuni zinazofanya vizuri sana katika swala zima la simu janja. Kumbuka OnePlus 3 tayari imeshateka soko kwa baadhi ya watu na ilikua imeachiwa mwezi wa 6 tuu.
OnePlus 4 kwa upande mwingine inategemewa kutolewa mwaka 2017. Simu janja hii itakuja na maboresho mengi ikiwemo na RAM ya GB 8, Pixel za Display kuboreshwa. Simu hii inasemekana kuja na MP 21 au 23 kwa kamera yake ya mbele na ile ya selfie itakua ni MP 12 au 16. Simu hii inategemewa kuwekwa sokoni mwezi wa 4 au 5 mwaka 2017
4. Samsung Galaxy S8
Kuna baadhi ya watu wameshakata tamaa na Samsung NOTE 7 baada ya matatizo ya kulipuka na kupata moto kutokea. Taarifa zilizopo ni kwamba simu janja ya Galaxy S8 itakuja ikiwa na kioo kilichojikunja.
Mategemeo ni kwamba itaanza kupatika mwezi wa pili mwaka 2017. Simu hii inasemekana kuwa itakuwa inasapoti uwezo wa 4K. Kujua mengi zaidi katika ndani ya simu hii endelea kutembelea TeknoKona kila siku kwani tutakupa taarifa zaidi pale tuu zitakapotufikia.
5. Xiaomi Mi 6
Simu janja za Xiaomi kwa china ndio simu zinazoongoza kwa mauzo. Kuna mwaka ziliuza sana na kwa haraka mpaka zikaingia katika rekodi ya dunia . kujua kuhusu hilo soma hapa
Simu janja hii ni baada ya Xiaomi Mi 5 na inatarajiwa kuwa na uwezo wa 4K na pia maboresho kadhaa katika Pixel, Prosesa. Inatarajiwa kuwa na MP 23 katika kamera ya nyuma na MP 7 katika kamera ya mbele au MP 21 kwa kamera ya nyuma na MP 13 kwa kamera ya mbele.
Xiaomi Mi 6 pia inasemekana itakuwa inasapoti huduma ya 5G, uwezo wa RAM ya GB 6 au 8. Betri kuwa la mAh 4,000 au 4,200 ujazo wa uhifadhi unaweza ukawa mwingi hadi GB 256.
Simu janja hii itakuwa ni ya aina yake kwani kampuni ya Xaiomi imewekeza nguvu nyingi sana katika simu hii. Simu hii ina vipengele vingi sana na sifa nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine zinaifanya simu hii kuweza kushindana na simu janja nyingine. Juu ya yote kubwa ni kwamba simu hii itakuwa pia inajitafutia njia katika soko la U.S
Usikae mbali na TeknoKona kwani kwa leo tumekuelezea juu juu kuhusiana na simu hizi. Japokuwa ndizo zinazosubiriwa kwa hamu zaidi, zikitoka tuu TeknoKona itakupa uchambuzi juu ya simu janja hizo,
Ningependa kusikia kutoka kwako wewe ni simu janja gani ambayo unaisubiria kwa hamu kabisa? Niandikie hapo chini sehemu ya comment