Apple kuja na toleo la Apple Watch lenye eneo la laini ya simu. Vyanzo vya ndani ya kampuni ya Apple vimekaririwa vikisema Apple wanatengeneza toleo la Apple Watch litakalokuja na eneo la laini ya simu.
Apple Watch kuja na eneo la laini ya simu. Â Mtandao maarufu wa Bloomberg umezipata taarifa hizi kupitia baadhi ya maafisa wa kampuni hiyo.
Tokea toleo la kwanza la saa janja za Apple Watch saa hizo zimekuwa zikiitaji kuwasiliana na simu ya iPhone kupitia mfumo wa bluetooth ili kuzipa uwezo wa kutuma na kusoma ujumbe mfupi wa sms, kutumia app ya ramani na ata kusikiliza muziki kutoka mtandaoni (stream).

Apple wanategemea kutumia mfumo wa teknolojia ya LTE ndani ya saa hizi na hivyo kuzipa uwezo wa kutumia laini za simu zenye intaneti ya kasi ya 4G.
Uamuzi huu unaonekana utawasaidia zaidi Apple kuweza kulifikia soko kubwa zaidi la saa janja. Uwepo wa ulazima wa kumiliki simu za iPhone ili kuweza kutumia Apple Watch limekuwa jambo linalokwamisha mauzo mengi ya saa hizo.
Vipi kwako? Je ushawahi kuvutiwa na matumizi ya saa janja? Tupe mtazamo wako.
Vyanzo: Business Insider na Bloomberg