fbpx
Afya

Afanyiwa upasuaji wa kutoa chaja ya simu mwilini

afanyiwa-upasuaji-wa-kutoa-chaja-ya-simu-mwilini
Sambaza

Mwanaume mmoja huko nchini India katika jimbo la Assam afanyiwa upasuaji wa kutolewa chaja ya simu mwilini mwake. Upasuaji huo ulitegemewa kuwa wa kawaida ila ukawa usio wa kawaida.

Afanyiwa upasuaji wa kutolewa chaja ya simu mwilini
Afanyiwa upasuaji wa kutolewa chaja ya simu mwilini

Mgonjwa huyo, mwanaume wa miaka 30 alienda akidai anasikia maumivu makala eneo la chini la tumbo na hii ni baada ya yeye kumeza chaja ya simu ya urefu wa futi 2. Ila mwisho wa siku ikaja kuonekana alidanganya, chaja hiyo ilikutwa kwenye kibofu cha mkojo.

INAYOHUSIANA  Je umeshawahi tumia poda ya JOHNSON'S !? Ina skendo ya kusababisha kansa ya kizazi!

Ilikuwaje:

Madaktari mwanzo walimpatia dawa za kuharisha wakidhani ataweza kutoa waya huo kupitia haja kubwa. Baada ya kuona haijatoka wakaamua kumfanyia vipimo vya X-ray. Hapo ndipo wakagundua ya kwamba mwanaume huyo alidanganya, waya huo upo kwenye kibofu cha mkojo.

Inasemekana mwanaume huyo ana tabia za ajabu za kingono zinazohusisha kujiingiza vitu kupitia uume wake.

 

Afanyiwa upasuaji wa kutolewa chaja ya simu mwilini

Madaktari walifanikiwa kumfanyia upasuaji na kuutoa waya huo. Kwa sasa anaendelea na matibabu na wanaamini atapona vizuri.

Vyanzo: HindustanTimes

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |