fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Kivinjari Kompyuta Maujanja Teknolojia

WhatsApp ya giza kwenye Chrome, Safari, FireFox

tecno

Kama kuna kipengele ambacho katika miezi ya karibuni kimepata umaarufu wa aina yake (hasa kwa wale ambao wanafahamu kitu hicho kipo ndani ya programu tumishi yenye watumiaji wengi zaidi) ni “WhatsApp ya Giza” lakini sasa mpango huo umeenda mbali zaidi na kupatikana kwenye kivinjari cha Google Chrome, Firefox, Safari, n.k.

Wengi wetu ambao tunamiliki simu janja basi ninaamini kuwa wewe ni mmoja wa watu wengi duniani ambao wanatumia WhatsApp kufanya mawasiliano na pengine unatumia toleo la karibuni ambalo lina kipengele cha muonekano wa giza au kwa lugha ya Kiingereza “Dark mode“.

SOMA PIA  CarbFix: Wanasayansi wageuza hewa ya sumu kuwa jiwe. #Sayansi

Sasa kama wewe ni kama mimi ambae tunatumia WhatsApp kupitia kivinjari (Safari, Opera Mini, Chrome) na umetokea kupendezwa na muonekano wa giza kwenye simu si vibaya ukafahamu kuwa kipengele hicho hivi sasa kimeruhusiwa kwenye WhatsApp Web ambayo unaweza kutumia kupitia kompyuta/kipakatalishi au hata simu ya kiganjani ingawa kufanikisha jambo hili lina ugumu wake kidogo lakini naamini maelezo yangu yatakufundisha na utafanikisha kuhama kutoka mwonekano wa mwanga mpaka giza.

tecno

 1. Hatua ya kwanza kabisa ni kutembelea tovuti husika>>>WhatsApp Web kisha kufungua WhatsApp ndani ya kifaa chako cha kiganjani na kubofya kwenye zile nukta 3 zinzoonekana upande wa kulia juu na kwenda palipoandikwa WhatsApp Web na kufungua msimbo kwa kutumia simu janja.
  WhatsApp ya giza

  Hatua ya awali kabisa kuweza kutumia WhatsApp Web.

   

 2. Mara bada ya mazungumzo yako ya kwenye WhatsApp ndani ya simu kuwa sawa na pale kwenye Chrome, Firefox sasa bofya kitufe cha pili kwenye kipanya kwa lengo la kupata menyu ndogo halafu chagua “Inspect” au shikilia Ctrl+Shift+I kwa pamoja kwenye kicharazio.WhatsApp ya giza
 3. Kwenye huo ukurasa mpya uliofunguka sasa kazi itakuwa ni moja tu; kutafuta neno body class=”web”. Kama unatumia kivinjari kiitwachwo Safari tafuta body class=”web text-rendering-bug-fix”. Ukifanikiwa kuliona neno husika bofya kile kitufe cha kulia kwenye kipanya kisha chagua “Edit as HTML“.
 4. Hariri kwa kuongeza neno dark mara tu baada ya web au body class=”web dark text-rendering-bug-fix”. Sasa malizia kwa kubofya “Enter” kutoka kwenye kicharazio.

  WhatsApp ya giza

  Muonekano wa WhatsApp ya giza kwenye kipakatalishi.

Lakini kama hatua hizo kwako ni changamoto kuweza kuzikumbuka ili kubadilisha muonekano wa WhatsApp kwenye kivinjari unaweza ukaongeza programu wezeshi  kama Stylish ambayo itafanya kile ambacho nimekielezea hapo juu. Ningependa kupata maoni yako iwapo maelezo yangu yamekusaidia kuhama kutoka muonekano mmoja hadi mwingine.

Chanzo: Gadgets 360

SOMA PIA  Tecno watambulisha Phantom 6 na 6 Plus; Na sasa Kupatikana Duniani kote
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania