Kampuni ya utengenezaji wa magari ya kijerumani ya Volkswagen inatarajiwa kutangaza mpango wake wa utakaosuruhisha mgogoro wake na vyombo vya mazingira vya Marekani ambao unasemekana utahusisha Volkswagen kununua magari ambayo iliyauza yakiwa na makosa katika uzalishaji wa hewa chafu.
Mgogoro wa Volkswagen na Mamlaka za mazingira Marekani.
Mwezi Septemba mwaka jana mamlaka za Marekani ziligundua kwamba magari yanayouzwa Marekani ya Volkswageni yalikuwa yanafungwa kifaa fulani ambacho kilikuwa kinatambua gari linapokuwa katika vipimo na kisha kubadili ufanisi wake ili liweze kufaulu vipimo hivyo.
Baada ya kugundua hivi VW wakakiri kwamba sio tu Marekani bali magari zaidi ya magari milioni 11 dunia nzima yalikuwa yamefungwa kifaa hiki, magari hayo yanajumuisha aina kadhaa ambazo hapa Afrika mashariki pia ni maarufu kama vile Audi A3 Golf, Beetle na Passat.
Mpango wa Volkswagen kupata suluhisho la mgogoro huu
Tetesi zilizolripotiwa na mtandao wa LA TIMES zinasema kwamba VW wameamua kutatua mgogoro huu kwa kuyatengeneza magari yote yaliyouzwa na kifaa hicho ili yaweze kufikia viwango vilivyowekwa na kwa magarai mengine watayanunua hili litategemea na uamuzi wa mmiliki wa gari.
Ingawa haijajulikana ni kwa namna gani VW itaweza kurekebisha magari ambayo yalikuwa hayakidhi viwango ila ni wazi kwamba hii ndio njia pekee hasa iliyobaki, inakadiriwa kwamba VW watatumia yapata dola za kimarekani kutengeneza magari yote ambayo yanashida pamoja na kuyanunua ambayo watumiaji wake watataka yanunuliwe. Kwa matoleo ya karibuni gharama za kurekebisha zitakuwa ndogo kwa kuwa ni upande wa software tu ndio ambao unashida lakini kwa matoleo ya zamani matengenezo hasa yanahitajika.
Yapo mengi ambayo Afrika mashariki inatakiwa kujifunza kutoka na sakata hili la VW kubwa ikiwa ni kusimamia sheria kwa mamlaka zinazohusika. Mamlaka za Marekani zilisimama imara baada ya kugundua kwamba VW wamekiuka taratibu hii imepelekea kwa watengenezaji hawa wa magari kutafuta ufumbuzi lakini pia wafanya biashara na wazalishaji wa Afrika mashariki wanatakiwa kuzingatia sheria zote zikiwamo za mazingira kwani ni muhimu kutunza mazingira yetu.