fbpx
Android, Apple, apps

VLC 3.0: VLC waleta sasisho kubwa zaidi, Download toleo jipya kwa simu, kompyuta n.k

vlc-3-0-vlc-waleta-sasisho-toleo-jipya
Sambaza

VLC waleta sasisho kubwa zaidi kufanyika katika miaka ya hivi karibuni. Toleo la VLC 3.0 ni toleo jipya la VLC kwa matumizi ya vifaa vya aina mbalimbali; Android, iOS, Windows OS, MacOS, Linux na Chrome OS.

Toleo hili ndilo toleo la kwanza linalohakikisha code ya utengenezaji wa app hiyo ni hiyo hiyo ilitumika katika utengenezaji wa matoleo mengine ya app hiyo kwa ajili ya matoleo ya programu endeshaji zingine zote.

INAYOHUSIANA  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Toleo la VLC 3.0 kwa kompyuta zinazotumia programu endeshaji ya Windows linakubali kwenye matoleo mbalimbali ya Windows kama vile XP, Vista, 7, 8, na Windows 10.

Kwa watumiaji wa iOS, toleo hili linakubali kuanzia vifaa vyenye toleo la iOS 7 na kuendelea.

Kwa wanaotumia simu za Android toleo hili linakubali ata kwenye simu zinazotumia matoleo ya zamani zaidi ya Android, kuanzia Gingerbread 2.3.

INAYOHUSIANA  Barua ya wazi: Ni miaka tisa sasa Android mpenzi!

Uwezo mwingine speshali ni ‘Chromecast; kwa watumiaji wa Android na Chromebooks’.

Chromecast ni nini?

chromecast ni nini
Chromecast ni nini?

Chromecast ni kifaa kidogo cha kuchomekwa kwenye TV kupitia teknolojia ya HDMI na inakuwezesha kurusha moja kwa moja kitu unachotazama kwenye simu, tableti au laptop na kikawa kinaonekana kupitia TV yako, uwezo huu unafanyika kupitia teknolojia ya Wifi ambayo simu na chromebook inazitumia kwa wakati huo.

Pakua/Download app ya VLC 3.0 kwa ajili ya kompyuta, simu, au tableti hapa -> Download VLC 3.0

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |