Suala la utumiaji wa simu na ugonjwa na kansa/cancer vimekuwa vikihusishwa sana. Lakini kulikuwa na kitu kimoja kilichokuwa kinakosekana, nacho ni utafiti mkubwa juu wa jambo hili.
Na sasa kutokana na utafiti wa muda mrefu nchini Denmark wa matumizi ya simu na matukio ya ugonjwa ya cancer imegundulika hivi vitu viwili havina mahusiano kama wengi tulivyokuwa tunaamini.
Kwa kutumia data muhimu za watu zaidi ya laki nne kati ya mwaka 1996 na 2002, kwa watumiaji na wasio watumiaji wa simu kuugua kwa ugonjwa huu hakujaonesha mahusiano yoyote na umilikaji wa simu. Hii ikimaanisha asilimia ya watu waliopata kansa katika kundi la wasiotumia simu halijapishana sana na asilimia kama hiyo katika watumiaji simu!
Kwa hiyo vijana kazi kwenu!!! Extreme kama kawa!
No Comment! Be the first one.