fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Teknolojia

Tujue Kwa Ufupi Historia Ya ‘KeyBoard’ Na Wapi Tunapoenda Na Teknolojia Hii!

Tujue Kwa Ufupi Historia Ya ‘KeyBoard’ Na Wapi Tunapoenda Na Teknolojia Hii!

Spread the love

Bila kuwa na ‘keyboard’ sijui tungeweza vipi tuma meseji zetu katika vifaa vyetu. Sema uzuri wa teknolojia ni kwamba wataalamu wangekuwa radhi kutafuta njia nyingine ya kutuwezesha kufanya hilo.

Sawa siku hizi unaweza ukatuma meseji kwa kuamuru kifaa chako kifanye hivyo kwa mdomo. Lakini ukiangalia katika sehemu pana zaidi ni kwamba haya yote yaliwezeshwa baada ya ugunduzi wa ‘keyboard’ kuchukua nafasi yake

Ngoja Tuangalie Tulipotokea, Mahali Tulipo Na Mahali Tunapoenda Na Teknolojia Hii

Hapo Awali
Hapo awali kabisa kabla mambo hayajakaribia hata kuwa kama yalivyo sasa, binadamu alitafuta njia mbali mbali kuweza kujielezea au hata kuelezea kitu. Kwa kipindi hicho njia kubwa ambayo ilikuwa ikitumika ilikuwa ni kwa kuchora. Baada ya lugha kugunduliwa basi binadamu akaanza kuweza kueleza/kujielezea kwa kutumia maneno

Watu walipojua kuandika na kadhalika, peni yao waliokuwa wanatumia kwa wakati huo ilikuwa ni ule upande wa chini wa nyoya (ule mgumu, ambapo nyoya linajiungia katika ngozi ya ndege).

Ilipogundulika hii watu walianza kuandika lakini watu walikuwa wanaandika kidogo ili kuelezea mambo yao tofauti tofauti. Licha ya kujielezea mambo machache machache lakini bado watu walikuwa na uwezo wa kuandika mambo yao – hii ilikuwa ni moja kati ya mambo yenye faida kubwa kwa mwanadamu—jinsi wanavyotaka.

SOMA PIA  Mambo Ma 5 Ambayo Hutakiwi Kuyaweka Wazi Facebook!

Baada Ya Hapo (Karne Ya 19)
Baada ya hapo, wataalamu wakagundua kifaa ambacho kitawawezesha watu kuandika ambacho kinakilikana kama ‘TypeWriter’ (mashine ya chapa). Kifaa hichi kilipogunguliwa ilikuwa ndio njia ya haraka ya kuandika mambo mengi kwa kutumia muda mchache.

MissIS

Kompyuta ilipogunduliwa basi wataalamu wakaona ‘TypeWriter’ (mashine ya chapa) iwe kama ‘Keyboard’ katika kompyuta na hilo likafanikiwa kwani ndio ilikuwa hivyo.

Sasa (Karne Ya 21)
Kwa karne hii watu tunatumia ‘Keyboard’ zile zenye mpangilio wa QWERTY kama herufi za mwanzo kabisa za kuanza nazo. Maswali yamezuka mengi sana kama vile kwanini namba za kwenye ‘Keyboard’ haziko katika mpangilio wa A – Z. Jibu ni moja tuu hapo, kama namba hizo zingekuwa katika mtiririko huo basi watu wengi wangekua wanatumia muda mwingi sana katika kuandika kwani mfumo huo ungekuwa hauokoi muda.

Muinuko Katika Herufi F na J

Muinuko Katika Herufi F na J

Swali la pili inawezekana ukawa hujawahi kulisikia — ila ukiangalia katika ‘keyboard’ ya kompyuta yako utanielewa – ambalo linauliza kuwa kuna maana gani nyuma ya vinundu vilivyo katika herufi F na J katika ‘keyboard’? Hakuna jibu lenye uzito mkubwa sana juu ya jambo hili licha ya vinundu hivyo kuwa vinatuwezesha kuweka mikono yetu vizuri katika keyboard tukianza kuandika kitu.

SOMA PIA  Facebook Inajaribu Utumiaji Wa Kamera Kama Ya Snapchat!

Hapo Mbeleni
Kuna hatihati kubwa sana ambazo zinaonyesha kuwa mfumo wa ‘keyboard’ wa QWERTY utabadilika. Makampuni ya simu janja nayo yameona mfumo huo wa QWERTY haujitoshelezi katika simu zao. Licha ya makampuni ya simu, kuna makampuni mengi tuu yamejikita kutengeneza ‘keyboard’ haswa haswa za simu katika njia ambayo wao wanaona ni rahisi zaidi na itawasaidia watu katika kuhakikisha wanaandika mambo yao kwa haraka zaidi.

Mfano kuna kampuni imeandaa ‘keyboard’ kwa watumiaji wa simu janja na tablet, ‘keyboard’ hiyo imepewa jina la Kalq.

Keyboard kutoka KALQ

Keyboard kutoka KALQ

Pia kuna ‘Keyboard’ kwa ajili ya skrini zinazotumia sense za vidole maarufu kama ‘Touch Screen’ mfano mzuri wa ‘keyboard’ hizi ni zile za Swype kutoka kampuni la Nuance. Mfumo huu wa ‘keyboard’ utamuwezesha mtumiaji wa kifaa kuwea kuandika mambo yake bila kundika kwa njia ya kawaida kama tulivyozoea. Yaani mtumiaji atahitaji kupitisha vidole vyake juu ya herefi zinazounda neno Fulani ili neno hilo lijiandike.

Mfano Wa Jinsi Ya Kuandika Neno 'Hello' Katika Keyboard Ya Swype

Mfano Wa Jinsi Ya Kuandika Neno ‘Hello’ Katika Keyboard Ya Swype

Lakini kwa haraka haraka ni kwamba mifumo hii kutoka kwa Kalq na Swype zitakuwa zikitumika san asana katika simu. Ukija katika kompyuta ambapo panajumuisha maandiko ya mambo mengi sana kama vile vitabu n.k teknolojia ambayo itafuata itakuwa ni ile ya kuongea. Yaani mtu utakuwa unaongea huku herufi zinajiandika zenyewe. Usishtuke hili linawezekana kumbuka mpaka sana kuna mambo kama vile Siri (kutoka Apple) na Cortana (Kutoka Microst) ambazo huduma hizi zote mbili unaweza ukaziamuru zifanye jambo Fulani kama vile kupiga simu kwa kutumia kinywa chako (sauti).

SOMA PIA  Obama atajua juu ya John Snow kabla yetu.

Sasa fikiria teknolojia kama hizi zikiwekwa katika ubunifu wa ‘Keyboard’ ambayo inaweza ikawa inapewa amri kwa mdomo juu ya maneno gani kuyaandika. Japo kuwa kwa upande wangu tatizo litakuwa ni kuweza kuufanya mfumo mzima kutambua lugha nyingi zaidi, lakini kwa kuanza kiingereza kitakuwa ndio baba lao kwa kushika usukani.

Ningependa kusikia kutoka kwako,nipe mawazo yako wewe unahisi ni kitu gani ambacho kinaweza kikawepo hapo baada katika ‘Keyboard’ ambacho mimi sijakisema. Niandikie sehemu ya comment hapo chini, Pia kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania