fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta

Surface Book: Microsoft na Uamuzi wa Kutengeneza Laptop Zake

Surface Book: Microsoft na Uamuzi wa Kutengeneza Laptop Zake

Spread the love

Kwa muda wa miaka mingi Microsoft imekuwa ikitengeneza programu endeshaji, Windows, na kisha kuwauzia wengine kama vile HP, Dell, Acer n.k ambao ndio wamekuwa wakitengeneza vifaa kama laptop na kompyuta mbalimbali zinazotumia programu endeshaji ya Windows. Mambo yanabadilika.

Kampuni ya Microsoft imeamua kuangia kwa nguvu kwenye utengenezaji wa vifaa kama vile Apple inavyofanya na laptop zake za MacBook.

Kwa miaka mingi wengi wamesema uzuri wa laptop kutoka kampuni ya Apple, yaani MacBooks, unatokana na kampuni hiyo kusimamia mambo yote – kuanzia utengenezaji wa programu endeshaji yao ya Mac OS hadi utengenezaji wa vifaa vya utumiaji wa programu hiyo – yaani MacBooks.

Microsoft Surface Book

Microsoft Surface Book

Na sasa Microsoft pia inajikita katika hilo kwa nia ya kuendelea kusimama katika soko. Jambo hili linaleta maana sana kwao kwa sababu pia hivi karibuni na ujio wa toleo la Windows 10 tayari wamesema hakutakuwa na toleo jingine tena, yaani Windows 11 – kutakuwa na masasisho (updates) tuu. Hii inamaana biashara ya kuuza matoleo ya programu ya Windows ndio inaondoka hivyo.

Surface Book

Surface Book pia inakuja na pen spesheli kwa ajili kutumika kwenye kioo chake mguso (touch screen)

Surface Book pia inakuja na pen spesheli kwa ajili kutumika kwenye kioo chake mguso (touch screen)

Surface Book ambayo ndiyo laptop yao ya kwanza wameitambulisha hivi karibuni na kwa kweli ni ya kiwango cha hali ya juu. Ni laptop inayoweza badilika na kuwa tableti pale unapoitaji. Yaani unaweza ikunja au ukachomoa eneo la keyboard kabisa.

SOMA PIA  Kompyuta: Ubora uleule lakini faili ni dogo

Surface Book inakuja katika matoleo mawili.

Moja inakuja na prosesa ya Intel Core i5 wakati nyingine inakuwa na prosesa ya Intel Core i7. Zote zinakuja na kadi ya ubora wa juu katika ‘Graphics’, nayo ni NVIDIA GeForce GPU.

Hadi sasa imepata sifa nyingi sana za kiubunifu. Angalia eneo linalojikunja pale unapoikunja. Unaweza ukaichomoa bila shida kuitengenisha na keyboard na ukaendelea kuitumia kama tableti

Hadi sasa imepata sifa nyingi sana za kiubunifu. Angalia eneo linalojikunja pale unapoikunja. Unaweza ukaichomoa bila shida kuitengenisha na keyboard na ukaendelea kuitumia kama tableti

Zina sehemu mbili za USB 3.0, na pia zinaeneo la kuchomeka memori kadi (SD Card). Uwezo wake wa chaji ni mkubwa, zina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa masaa 12, hili litawafanya Apple, watengenezaji wa MacBooks kukuna kichwa zaidi wakiwa wanatengeneza MacBooks zijazo.

  • Diski ujazo – Kutakuwa na GB 128, GB 256, GB 512, au TB 1. katika mfumo wa SSD.
  • Ukubwa – Inchi 13.5
  • Ukinunua toleo la i5 utapata RAM ya GB 8 wakati toleo la i7 linakuja na RAM ya GB 16. Hivi ni viwango vikubwa na vizuri vya RAM kwa laptop yeyote ya kisasa.
SOMA PIA  Vifaa vya kielektroniki vinavyo tengenezwa na Apple

Na Microsoft wanadai laptop zao hizi za Surface Book zinanguvu mara mbili ukilinganisha na zile za MacBook Pro zinazotengenezwa na Apple.

Bei ya Surface Book ya inaanzia kwenye milioni 3.2-3.5 za Kitanzania.

Uamuzi wa Microsoft kuingia katika eneo la utengenezaji laptop umesifiwa na wengi huku wengi wakiona ni jambo litakalozidisha kukuza ubunifu katika laptop zinazotumia programu endeshaji ya Windows.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania