Hiki ni kitu kimojawapo ambacho watu hawakudhania kabisa, tulifikiria ndio toleo la mwisho –la Playstation 5 ambalo tayari lipo—lakini kampuni ya Sony imekuja kutushangaza.
Ni wazi kuwa soko la magemu ni soko ambalo lina mapato mengi sana na licha ya hivyo ni kwamba linakua kwa kasi sana na kwa miaka mingi Playstation kupitia Sony imeonekana ikishika usukani.

Kama ulishaizoea Playstation 5 ambayo tayari ipo sokoni na inatumika na watu wengi, pata picha kuona toleo lingine kabisa ambalo bado halipo sokoni hivi karibuni.
Muonekano mpya utakua na rangi ya kijivu jivu hivi na pia itakua inakuja na vifaa vitatu yaani padi, spika za masikio (Headphone) na kifaa cha PS yenyewe.
Hapa ni kwamba muonekano wa PS unakua haujabadilika sana ukaichana na kuwa na rangi ya kijivu tuu.

Wateja watanzaa kutoa oda za mwanzo ifikapo tarehe 15 septemba lakini vifaa hivi vitaanza patikana duniani kote mpaka kufikia oktoba 14.
Unaweza kupata vifaa hivyo kwa kupitia direct.playstation.
Wale ambao wanategemea kuuza reja reja kwenye maduka yao wataanza kupata vifaa hivyo ifikapo tarehe 28 oktoba mwaka huu.
Hii itaongezeka katika zile rangi za PS 5 ambazo zilikua zimeshatoka tayari, na ukifikiria kwa undani labda Sony wamefanya hivi makusudi kabisa.
Kusudi lao likiwa ni kuhakikisha kuwa inaongeza mauzo ya vifaa hivyo vya Playstation 5 kwa uraharaka zaidi iwezekanavyo.

Soko la michezo/magemu ni soko ambalo linaingiza mapato mengi sana kwa mwaka na makampuni mengi yameshaliona hilo.
Kumbuka tumeshaandika kuhusiana na magemu ya Playstation kuanza kupatikana katika simu janja….soma zaidi >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako,niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unahisi ni sawa kama kampuni kuja na kifaa kingine chenye rangi nyingine wakati tayari walishatoa kifaa chenye rangi nyingine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.