Inajulikana kuwa Playstation 5 ni moja katika ya vifaa vya magemu ambavyo ni maarufu sana kwa sasa. Kingine ni kwamba Playstation ni moja kati ya vifaa vinavyoingiza pesa nyingi katika kampuni ya sony.
Tuliandikana >>HAPA<< ingia kusoma zaidi, lakini licha ya hayo yote bado kampuni ina mpango wa kujikuza zaidi na kuhakikisha kuwa magemu yake yanapatikana maeneo mbali mbali.
Hatua hii ni nzuri sana hasa kwa huduma ya Playstation Plus ambapo itakua inapatikana hata nje ya kifaa cha Playstation 5.
Yaani ni kwamba gemu zitaanza kupatikana katika vifaa mbali mbali na sio lazima kifaa hicho kiwe ni Playstation (Playstation 5).

Monitor hizi ni mpya ni moja ya njia ya kampuni kujikuza na kufikia watu wengi zaidi ukilinganisha na hapo awali. Inategemewa kuwa ni bidhaa inayoweza kutumiwa na ata wacheza magemu wanaotumia vifaa vingine, kama vile kompyuta.
Sifa za M9
- Ukubwa wa inchi 27
- Kiwango cha ubora onyeshi wa 4K, 144HZ
- Inakuja na port mbili za HDMI 2
Bei inaweza ikawa ni changamoto kiasi, kwani hii inauzwa kwa Dola 899, takribani Tsh 2,097,000/=. Kwa bei hiyo mtu anaweza kupata mbadala kwa bei nafuu zaidi, na kwa ukubwa zaidi.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, Je hili umelipokeaje? Je utakua tayari kuanza kutumia Monitor hizi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.