Kampuni ya Infinix imetangaza kuja na teknolojia ya kuchaji simu kwa nguvu ya Watt 180 itakayoitwa Thunder Charge. Kiasi hicho cha nguvu ni ongezeko kutoka katika kiasi cha mwisho kilichotolewa na kampuni hio, Watt 150, na kiasi hicho cha nguvu kinatarajiwa kujaza betri yenye ukubwa wa 4500 mAh ndani ya dakika nne tu!
Ndio, dakika nne tu. Infinix watatumia betri za aina ya 8C, ambapo zitakuwa mbili, zilizoungwa kwa kufuatana ili kila moja iweze kuchaji kwa nguvu ya Watt 90 tu. Kampuni hio imeshirikiana na makampuni makubwa ya kutengeneza betri ili kutengeneza betri ambayo itakuwa na ukinzani wa umeme uliopunguzwa kwa takribani asilimia 50. Hili litasaidia kuingiza umeme haraka zaidi katika betri. Pia wameweka namna mbalimbali za ulinzi wa kimfumo na katika vifaa ili kusaidia betri kutohaaribika kutokana na nguvu hii kuwa. Idadi ya namna hizo ni mia moja na kumi na moja (111).
Wameweka sensa ishirini za joto, katika maeneo mbalimbali kama betri, sehemu ya kuchomeka waya wa chaji , lengo ikwa ni kuhakikisha simu haizidi nyuzijoto 43 wakati ikiwa inachaji. Kama katika toleo lao la Infinix Note 12 VIP, mtumiaji ataweza kuamua kuruhusu nguvu kamili kupitia muundo wa kuchaji wa Furious au ataweza kuweka muundo wa kawaida (Normal), ili ichaji kwa nguvu ya chini, ila ambayo bado ina kasi kubwa.
Kampuni ya Infinix pia itaweza kuruhusu vifaa vingine kuchajiwa kwa chaja yenye uwezo huo wa watt 180, ila nguvu katika matumizi kama hayo itaishia kiasi cha Watt 90 mpaka Watt 100. Ili kuhakikisha waya unaotumika kuchaji utaweza kupitisha umeme katika nguvuhio kubwa, kampuni hio itaweka kifaa cha kuthibitisha waya unaotumika ili kuzuia uharibifu.
Kampuni ya Infinix inapanga kutoa Simu ya kwanza yenye teknolojia hiyo baadae mwaka huu.
Nini maoni yako juu ya teknolojia hii Pamoja na teknolojia nzima za kuchaji simu kwa ujumla wake? Toa maoni yako sasa kupitia akaunti zetu za mitandao ya kijamii.
Chanzo: TechAdvisor
No Comment! Be the first one.