fbpx
apps, Mtandao wa Kijamii, Snapchat

Maelfu ya watumiaji wa app ya SnapChat hawajapendezwa na sasisho jipya

snapchat-maelfu-ya-watumiaji-wa-app-ya-snapchat-hawajapendezwa-sasisho-jipya
Sambaza

Snapchat ni moja ya app maarufu ya mtandao wa kijamii, na yenye umaarufu mkubwa zaidi kwa vijana duniani kote. Maelfu ya watumiaji wa app ya Snapchat hawajapendezwa sasisho jipya la app hiyo, lililokuja na mabadiliko mapya ya kimuonekano.

watumiaji wa app ya SnapChat hawajapendezwa na sasisho jipya

Maelfu ya watumiaji wa app ya SnapChat hawajapendezwa na sasisho jipya, kuna mabadiliko makubwa ya kimuonekano ndani yake.

Sasisho hilo jipya la Snapchat lililotolewa takribani wiki moja iliyopita, limeleta mabadiliko makubwa zaidi ndani ya app hiyo tokea ujio wa app hiyo mwaka 2011.

Snapchat ni app inayotumiwa kwa kasi sana na vijana, kwa wastani vijana wengi wanatumia muda mwingi zaidi katika app hii kuliko app zingine kama vile Instagram, Facebook na Twitter.

Nini kimebadilika;

Muonekano wa sehemu zote za app hiyo

– Mambo yanayowekwa na marafiki sasa yanapatikana upande wa kushoto wa app hiyo

– Habari na vingine vyovyote vinavyopostiwa na vyombo vya habari pamoja na matangazo, vinapatikana upande wa kulia

Watumiaji wa app hiyo wamesema kwa sasa imekuwa vigumu zaidi watu kupata au kuona mambo yalitumwa na baadhi ya marafiki zao.

INAYOHUSIANA  WhatsApp kutuma data zako kwenda mtandao wa Facebook!

Ombi kwenda kwa Snapchat kuwaomba wabadilishe sasisho hilo jipya na kurudisha muonekano wake wa zamani limewekwa kwenye mtandao wa Change.org na hadi sasa limewekwa sahihi na watu zaidi ya nusu milioni.

Vijana wengi zaidi wameendelea kutoa lawama kali dhidi ya Snapchat kupitia mtandao wa Twitter na kuna ambao ata wametishia kuachana na app hiyo maarufu.

Ni mara nyingi sana app au huduma za mtandao zinazokuja na mabadiliko ujikuta katika lawama kwani watu wanakuwa wameshazoea kitu flani kwa muda mrefu sana, ila haijawahi kutokea lawama hizo kuwa katika mamilioni na kwa mfululizo wa siku nyingi kama ilivyotokea kwa Snapchat.

Je watakubali??? 

Hii inaweza ikawa vigumu, inasemakana mabadiliko haya wameyaleta si tu katika kuboresha muonekano wa app hiyo bali pia ili kuboresha huduma kwa watangazaji matangazo pia ili kukuza mapato yake.

Je wewe ni mtumiaji wa app ya Snapchat? Tuambie maoni yako, je umependezwa na muonekano mpya?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |